[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Uzbekistan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
O‘zbekiston Respublikasi
O‘zbekiston Jumhuriyati
Ўзбекистон Республикаси

Jamhuri ya Uzbekistan
Bendera ya Uzbekistan Nembo ya Uzbekistan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: Wimbo la Taifa
Lokeshen ya Uzbekistan
Mji mkuu Tashkent
41°16′ N 69°13′ E
Mji mkubwa nchini Tashkent
Lugha rasmi Kiuzbeki
Serikali Jamhuri
Shavkat Mirziyoyev
Abdulla Aripov
Uhuru

Ilitangazwa
Formation
Recognized
Completed
1747 kama Dola la Bukhara,
Dola la Kokand, Khwarezm
1 Septemba 1991
8 Desemba 1991
25 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
448,978 km² (ya 56)
4.9
Idadi ya watu
 - Julai 2019 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
32,768,725 (ya 41)
74.1/km² (ya 132)
Fedha Som ya Uzbekistan (UZS)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
UZT (UTC+5)
not observed (UTC+5)
Intaneti TLD .uz
Kodi ya simu +998

-


Uzbekistan ni jamhuri ya Asia ya Kati.

Imepakana na Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Turkmenistan.

Mji mkuu na pia mji mkubwa ni Tashkent.

Madrasa ya "Sherdor" mjini Samarkand

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Uzbekistan ni nchi yenye historia ndefu. Ferghana, Tashkent, Bukhara, Khwarezm na Samarkand zilikuwa vitovu vya utamaduni wa binadamu tangu milenia ya 2 KK.

Katika karne kabla na baada ya Kristo eneo lilijulikana kama Sogdiana na Baktria. Miji yake ilikuwa na utajiri kutokana na biashara ya misafara kwenye barabara ya hariri kati ya China na Mashariki ya Kati.

Baadaye ilitawaliwa na milki mbalimbali za nje kama Uajemi.

Kuanzia uenezi wa Uislamu watu ba Uzbekistan waligeukia dini hiyo mpya.

Katika karne ya 14 jemadari Timur alijenga milki kubwa na kuharibu nchi za magharibi hadi Uturuki. Alipamba mji mkuu wake Samarkand kwa majengo mazuri.

Baada ya Timur milki yake iliporomoka na Uzbekistan ilitawaliwa na madola mbalimbali ya kieneo yaliyokuwa hasa eneo la mji muhimu.

Katika karne ya 19 Urusi ulieneza athira yake kuelekea kusini na kuunganisha madola ya Uzbekistan na milki yake.

Baada ya mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917 Uzbekistan ikawa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi kuporomoka kwake mwaka 1991. Ilijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiuzbeki" hadi 1991.

Tarehe 31 Agosti 1991 ilijitangaza huru na kudai kufuata demokrasia na kuelekea soko huria, lakini hadi sasa haki za binadamu haziheshimiwi sana.

Kuna wakazi 32,768,725 (2019).

Walio wengi (zaidi ya 83%) hutumia lugha ya Kiuzbeki ambacho ni kati ya lugha za Kiturki na ndiyo lugha rasmi. Angalia pia orodha ya lugha za Uzbekistan.

Kuna makundi mengi vidogo zaidi vya utamaduni tofauti kama vile Watajiki (4.8%), Wakazakhi (2.5%), Warusi (2.3%), Wakarakalpaki (2.2%), Watartari (1.5%), Wakorea (1,1%) na mengine.

Upande wa dini, 88.6% ni Waislamu, lakini wengi wao hawana madhehebu maalumu; Wasuni ni 18% na Washia 1%. Wakristo ni 9.4%, wengi wakiwa Warusi Waorthodoksi; Waprotestanti na Wakatoliki hawafikii 3%.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Uzbekistan travel guide kutoka Wikisafiri

Taarifa za jumla
Vyombo vya habari

Vyanzo vingine

[hariri | hariri chanzo]
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uzbekistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.