[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Vibanzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vibanzi na nyama.
Vibanzi na samaki.
Samaki na vibanzi.

Vibanzi (na majina mengine mengi kama vihepe, vibendo na chipsi kutoka Kiingereza "chips") ni aina ya chakula kinachotayarishwa kwa viazi au viazi vikuu.

Katika uandaaji wa chakula hiki viazi hukatwa kwa vipande vyembamba vilivyooshwa na kuwekwa kwenye mafuta ili viweze kuiva na kuliwa. Kwa kawaida hukaangwa mara mbili, mara ya kwanza kwa nyuzijoto °C 140 - 180 hadi kushika rangi nyeupe-njano. Baada ya kupoa kuwekwa katika mafuta yenye nyuzijoto 190 - 200 na kushika rangi ya njano-kidhahabu.

Katika nchi nyingi kun viwanda vinavyotengeneza vibanzi kwa wingi kwa ajili ya matumizi ya hoteli. Hapa viazi hukatwa kwa mashine kubwa na kukaangwa mara ya kwanza, halafu kugandishwa kwa nyuzijoto chini ya sifuri na kuuzwa kupitia maduka penye friza.

Chakula hiki hakina virutubishi vya kutosha kunufaisha sana mwili.

Kinyume chake, mara nyingi tunashauriwa kutokula chakula hiki kwani kinapikwa kwa mafuta mengi na mafuta hayo yanaweza kusababisha matatizo katika miili yetu tunapokula chakula hiki mara kwa mara.

Tunashauriwa sana kula vyakula vya asili visivyokuwa na mafuta mengi ili kujenga miili yetu kwa sababu mafuta yakiwa mengi mwilini yanaweza kusababisha matatizo kama vile ugonjwa wa moyo.pia huleta maradhi ya figo na hufanya mwili kuwa dhaifu wanasayansi walishauli kuwa ni heli kwa siku moja ukala kipande kimoja cha tikiti kuliko kula mfuko mmoja wa vibanzi

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vibanzi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.