[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Msekwoya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sequoia)
Msekwoya
Msekwoya mkubwa (Sequoiadendron giganteum)
Msekwoya mkubwa (Sequoiadendron giganteum)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Gymnospermae (Mimea isiyotoa maua)
Divisheni: Pinophyta (Mimea iliyo na matunda kwa umbo wa koni)
Ngeli: Pinopsida (Mimea kama msonobari)
Oda: Pinales (Miti kama msonobari)
Familia: Cupressaceae (Miti iliyo na mnasaba na msanduku)
S.F. Gray
Nusufamilia: Sequoioideae (Miti inayofanana na msekwoya)
Saxton
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 3:

Misekwoya (pia: miti mbao-nyekundu) ni miti ya nusufamilia Sequoioideae katika familia Cupressaceae (misanduku) ya oda Pinales (mikoni).

Miti hiyo ndiyo mikubwa zaidi duniani, ila kwa sasa takriban spishi zote za misekwoya zipo hatarini kutoweka.

Kuna jenasi tatu katika nusufamilia hiyo: Sequoia na Sequoiadendron katika majimbo ya Marekani Kalifornia na Oregon na Metasequoia katika Uchina.

Miti ya Sequoia na Sequoiadendron inajulikana kuwa mikubwa na mirefu kabisa duniani. Lakini Metasequoia ni miti midogo ikilinganishwa na ile mingine.

Miti hiyo ni “pyrophytes”, yaani inaweza kuishi katika mioto ya misitu kwa sababu Sequoioideae ina gome ambalo linapinga moto[1]. Kwa kweli, miti ya Sequoioidaea inatumia moto wa msitu kueneza mbegu. Mbegu ya Sequoioideae zinahitaji moto wa msitu kufungua na kukua. Kwa hiyo, Sequoioideae inahitaji moto wa msitu. Kwa kweli, mazoea ya kudhibiti moto yameumiza Sequoioideae kwa sababu inahitaji moto wa msitu kuzaliana. Kwa kuongeza, kila familia ya Sequoioidaea inatishiwa na hapana moto wa msitu, kutema magogo, uchafuzi wa hewa, na mabadiliko ya tabianchi[2].

Sequoioideae ni spishi za zamani sana. Spishi za kwanza za Sequoioideae zilikuwepo katika kipindi cha Jurassic[3]. Wanasayansi wanaamini Sequoioideae ina miaka milioni mia mbili kumi na tano.

Sequoioideae Mti katika California, Marekani

Spishi mbili za Sequoioideae katika California na Oregon zinaweza kupatikana upande wa magharibi wa safu ya milima ya Sierra Nevada. Spishi hizo zinapendelea kuwa katika misitu ya pwani kama “Cloud forest” ya pwani magharibi mwa Marekani[4].

Katika Uchina, Metasequoia inaweza kupatikana katika manispaa ya Chongquing kusini mwa kati mwa Uchina. Katika Uchina hakuna watu ambao wameona Metasequoia kwa muda mwingi kwamba watu walidhani miti ya Metasequoia imepotea. Mpaka mwaka 1943, wakati msimamizi wa msitu alitafuta Metasequoia katika milima ya mkoa wa Hubei[1].

Uhifadhi

[hariri | hariri chanzo]

Tangu mapema karne ya 19, Sequoioideae imehifadhiwa ndani ya mbuga za umma, bustani za mimea, na misitu ya kitaifa. Kwa sababu hiyo, Sequoioideae inaweza kupatikana katika nchi kama Ujerumani, Uingereza, Australia, na Zealand Mpya. Katika Zealand Mpya, kuwa hektari elfu tano na mia sita za msitu wa Mti Mwekundu[5]. Haswa, msitu huu una miti ya Sequoia kutoka California.

Metasequoia katika Uchina

Katika mwaka 1918, zaidi ya miaka mia moja iliyopita, John Campbell Merriam, Madison Grant, na Henry Fairfield Osborn walianzisha Ligi ya Kuokoa Miti Myekundu[6]. Ligi hii inalinda miti myekundu kwa kununua ardhi na kutengeneza mbuga kutumia ardhi hii. Ligi inatumia michango ya watu, serikali, na mashirika kununua ardhi. Tangu mwaka 1918, Ligi ya Kuokoa Miti Myekundu imeokoa eka laki mbili za ardhi ya msitu[7].

  1. 1.0 1.1 USDA, ARS, Germplasm Resources Information Network. "Sequoia sempervirens - Wikispecies". species.wikimedia.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-02.{{cite web}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  2. "The Threats to the Redwoods". Save the Redwoods League (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
  3. Ahuja M. R. and D. B. Neale. 2002. Origins of polyploidy in coast redwood (Sequoia sempervirens) and relationship of coast redwood (Sequoia sempervirens) to other genera of Taxodiaceae
  4. "Cloud forest", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-11-11, iliwekwa mnamo 2019-12-02
  5. "Welcome to The Redwoods - Whakarewarewa Forest, Rotorua, New Zealand". The Redwoods - Whakarewarewa Forest, Rotorua, New Zealand (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
  6. "Stephen T. Mather: A League and National Parks Trailblazer". Save the Redwoods League (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
  7. "Mission and History". Save the Redwoods League (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Msekwoya kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.