Lupus
Lupus | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Matamshi | |
Kundi Maalumu | Rheumatolojia |
Dalili | viungo vinavyouma na vinavyovimba, homa, maumivu ya kifua, kupoteza nywele, vidonda vya mdomoni, kuvimba kwa nodi za limfu, kuhisi uchovu, upele mwekundu[1] |
Miaka ya kawaida inapoanza | Umri wa miaka 15-45[1][2] |
Muda | Kwa muda mrefu[1] |
Visababishi | Si wazi[1] |
Njia ya kuitambua hali hii | Kulingana na dalili na vipimo vya damu[1] |
Dawa | NSAID (dawa zisizo za steroidi), corticosteroids, immunosuppressants, hydroxychloroquine, methotrexate[1] |
Utabiri wa kutokea kwake | Uhai wa miaka 15 ~ 80%[3] |
Idadi ya utokeaji wake | 2–7 kwa kila 10,000[2] |
Lupus, kitaalamu hujulikana kama systemic lupus erythematosus (kifupi: SLE), ni ugonjwa wa autoimmune, ambapo mfumo wa kingamwili hushambulia kimakosa tishu zenye afya katika sehemu nyingi za mwili.[1] Dalili zake hutofautiana kati ya watu na zinaweza kuwa chini hadi kali sana.[1] Dalili zake za kawaida ni pamoja na maumivu na kuvimba kwa viungo, homa, maumivu ya kifua, kupoteza nywele, vidonda vya mdomo, kuvimba kwa nodi za limfu, kuhisi uchovu na upele mwekundu ambao mara nyingi hupatikana kwenye uso.[1] Mara nyingi kuna vipindi vya ugonjwa huu kuwa mkali (flares), na vipindi vya kupokuwepo dalili zake (remission) ambapo kuna dalili chache tu.[1]
Sababu zake haziko wazi [1] na inafikiriwa kuhusiana na jeni pamoja na mambo ya kimazingira.[4] Miongoni mwa watoto mapacha wanaofanana, ikiwa mmoja wao ameathiriwa, kuna uwezekano wa 24% kwaba huyo mwingine ataathiriwa pia.[1] Homoni za jinsia za kike, mwanga wa jua, uvutaji sigara, upungufu wa vitamini D na maambukizo fulani pia yanaaminika kuongeza hatari zake.[4] Mfumo huu unahusisha mwitikio wa kinga ambapo kingamwili hushambulia tishu za mtu mwenyewe.[1] Hizi kwa mara nyingi ni kingamwili za kupambana na nyuklia na husababisha kuvimba.[1] Utambuzi wake unaweza kuwa mgumu na unategemea mchanganyiko wa dalili na vipimo vya maabara.[1] Kuna idadi ya aina nyingine za lupus erythematosus ikiwa ni pamoja na lupus erithematosus, ugonjwa wa lupus ya ngozi ya mviringo (discoid lupus erythematosus), na ugonjwa wa lupus wa ngozi wa muda wa kati (subacute cutaneous lupus erythematosus).[1]
Ugonjwa huu hauna tiba, na matibabu yake yanaweza kujumuisha dawa zisizo za steroidi (NSAIDs), kortikosteroidi (corticosteroids), dawa za kuzuia mfumo wa kinga (immunosuppressants), hidroksiklorokwini (hydroxychloroquine) na methotrexate.[1] Ingawa kortikosteroidi (corticosteroids) hufanya kazi vizuri kwa haraka, matumizi yake ya muda mrefu husababisha madhara.[5] Dawa mbadala haijaonyeshwa kuathiri ugonjwa huu.[1] Umri wa kuishi ni mdogo kati ya watu wenye SLE.[6] SLE huongeza kwa kiasi kikubwa hatari ya ugonjwa wa moyo na mishipa, na hii ikiwa sababu ya kawaida ya kifo.[4] Kwa matibabu ya kisasa, karibu 80% ya walioathiriwa wanaishi zaidi ya miaka 15.[3] Wanawake walio na lupus wana mimba ambazo ni hatari zaidi lakini nyingi zake hufanikiwa.[1]
Kiwango cha SLE hutofautiana kati ya nchi kutoka 20 hadi 70 kwa kila 100,000.[2] Wanawake wa umri wa kuzaa huathirika mara tisa mara nyingi zaidi kuliko wanaume.[4] Ingawa kwa kawaida huanza kati ya umri wa miaka 15 na 45, aina mbalimbali za umri zinaweza kuathirika.[1][2] Wale wenye asili ya Kiafrika, Karibea, na Wachina wako katika hatari zaidi kuliko watu weupe.[4][2] Viwango vya magonjwa katika nchi zinazoendelea havijulikani wazi.[7] Lupus ni neno la Kilatini linalomaanisha "mbwa mwitu": ugonjwa huu ulipewa jina hili katika karne ya 13, kwani upele huu ulifikiriwa kwamba una mwonekano kama ule wa kuumwa na mbwa mwitu.[8]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 1.17 1.18 1.19 "Handout on Health: Systemic Lupus Erythematosus". www.niams.nih.gov. Februari 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Juni 2016. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 Danchenko, N.; Satia, J.A.; Anthony, M.S. (2006). "Epidemiology of systemic lupus erythematosus: a comparison of worldwide disease burden". Lupus. 15 (5): 308–318. doi:10.1191/0961203306lu2305xx. PMID 16761508.
- ↑ 3.0 3.1 The Cleveland Clinic Intensive Review of Internal Medicine (tol. la 5). Lippincott Williams & Wilkins. 2012. uk. 969. ISBN 9781451153309. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 13 Juni 2016.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 Lisnevskaia, L; Murphy, G; Isenberg, D (22 Novemba 2014). "Systemic lupus erythematosus". Lancet. 384 (9957): 1878–88. CiteSeerX 10.1.1.1008.5428. doi:10.1016/s0140-6736(14)60128-8. PMID 24881804.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Davis, Laurie S.; Reimold, Andreas M. (Aprili 2017). "Research and therapeutics—traditional and emerging therapies in systemic lupus erythematosus". Rheumatology. 56 (suppl_1): i100–i113. doi:10.1093/rheumatology/kew417. PMC 5850311. PMID 28375452.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Murphy, G; Isenberg, D (Desemba 2013). "Effect of gender on clinical presentation in systemic lupus erythematosus". Rheumatology (Oxford, England). 52 (12): 2108–15. doi:10.1093/rheumatology/ket160. PMID 23641038.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Tiffin, N; Adeyemo, A; Okpechi, I (7 Januari 2013). "A diverse array of genetic factors contribute to the pathogenesis of systemic lupus erythematosus". Orphanet Journal of Rare Diseases. 8: 2. doi:10.1186/1750-1172-8-2. PMC 3551738. PMID 23289717.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ Chabner, Davi-Ellen (2013). The Language of Medicine. Elsevier Health Sciences. uk. 610. ISBN 978-1455728466. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-07. Iliwekwa mnamo 2020-08-04.