Harakati
Mandhari
Harakati (kutoka neno la Kiarabu) mara nyingi hutumika kwa maana ya mchakato wa mtu au kundi la watu ambao wamejitoa kwa ajili ya kufuatilia jambo fulani, hususani katika jamii.
Katika harakati wahusika wanaojishughulisha nazo huwa wanajulikana kama wanaharakati kwa wingi wao, kama ni mmoja huitwa mwanaharakati.
Mara nyingi katika jamii ya watu wanaharakati hutumia muda wao mwingi katika kufuatilia mambo hayo. Kumekuwa na makundi mengi ya wanaharakati katika jamii yetu, kwa mfano kumekuwepo wanaharakati mbalimbali kama vile wanaharakati wa masuala ya uchumi, siasa, jamii na kadhalika.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |