[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Funafuti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Funafuti kwa macho ya ndege
Barabara kwenye sehemu nyembamba ya Funafuti (kushoto: bahari, kulia: bwawa la ndani ya atolli)
Shule ya Funafuti

Funafuti ni mji mkuu wa nchi ya visiwa ya Tuvalu. Ina wakazi 4,492 (mwaka 2002). Mji upo kwenye atolli ya Funafuti ambayo inafanywa na visiwa zaidi ya 30 ambavyo ni vyembamba vikiwa na upana kati ya mita 20 hadi 400 pekee.

Wenyeji huishi katika vijiji 9 ambavyo pamoja hufanya mji wa Funafuti. Majengo ya serikali ya nchi yanapatikana kwenye kisiwa kikubwa cha atolli kinachoitwa Fongafale chenye kijji cha Vaiaku (wakazi 682).

Kuna uwanja wa ndege, hoteli (Hoteli ya Vaiaku Langi), majengo ya kiutawala, na vile vile makazi. Nyumba za watu hujengwa kwa kufuata utamaduni wa jadi kwa viunga vya mitende, na hivi karibuni pia kwa kutumia bloku za saruji. Jengo maarufu zaidi kwenye atolli ya Funafuti ni Kanisa la Tuvalu.

Visiwa katika Funafuti

[hariri | hariri chanzo]

Kuna angalau visiwa 33 kwenye atolli. Kubwa zaidi ni Fongafale, ikifuatiwa na Funafala. Angalau visiwa vitatu vinakaliwa, ambayo ni Fongafale, Funafala na Motuloa.

  • Amatuku
  • Avalau
  • Falaoigo
  • Fale Fatu (au Falefatu)
  • Fatato
  • Fongafale
  • Fuafatu
  • Fuagea
  • Fualefeke (au Fualifeke)
  • Fualopa
  • Funafala
  • Funamanu
  • Luamotu
  • Mateika
  • Motugie
  • Motuloa
  • Mulitefala
  • Nukvalevale
  • Papa Elise (au Funangongo)
  • Pukasavilivili
  • Te Afuafou
  • Te Afualiku
  • Tefala
  • Telele
  • Tengako (peninsula ya kisiwa cha Fongafale)
  • Tengasu
  • Tepuka
  • Tepuka Vili Vili
  • Tutanga
  • Vasafua
  • And at least 5 other islands

Bwawa la ndani TeNamo

[hariri | hariri chanzo]

Bwawa la ndani ya atolli hujulikana kwa jina la TeNamo. Eneo lake la maji ni mnamo km2 275, ilhali eneo la nchi kavu linalozuguka bwawa la ndani ni chini ya km2 3.

8°31′S 179°13′E