Kalisi
Kalisi ni elementi na metali ya udongo alkalini yenye namba atomia 20 kwenye mfumo radidia ina uzani atomia 40.078. Alama yake ni Ca. Jina linahusiana na neno la Kilatini calx (mawe ya chokaa).
Kalisi | |
---|---|
Jina la Elementi | Kalisi |
Alama | Ca |
Namba atomia | 20 |
Mfululizo safu | metali ya udongo alikalini |
Uzani atomia | 40.078 |
Densiti | 1.55 |
Ugumu (Mohs) | 1.75 |
Kiwango cha kuyeyuka | 1115 K (842 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 1757 K (1484 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 3.39 % |
Hali maada | mango |
Tabia
haririKalisi ni kati ya elementi zinazopatiikana kwa wingi duniani, ikiwa na nafasi ya tano: asilimia 3.39 za ganda la dunia ni kalisi. Ikisafishwa hutokea kama metali laini yenye rangi nyeupe-fedha.
Inamenyuka rahisi kikemia hivyo haitokei kama elementi tupu lakini kwa kampaundi mbalimbali hasa katika mawe.
Unga wa kalisi au vipande vidogo vya metali huungua moto wenye rangi ya njano-nyekundu, unga hata bila kuwashwa kwa kumenyuka hewani tu.
Kalisi ni muhimu kwa miili ya wanadamu na wanyama, pia kwa mimea, kwa sababu inajenga mifupa na meno. Ina pia kazi katika mishipa.
Matumizi
haririKalisi ni muhimu sana katika maisha ya jamii. Ujenzi hutegemea sana kalisi na kampaundi zake. Mawe ya chokaa yaliwahi kutumiwa kwa ujenzi wa nyumba tangu miaka elfu kadhaa.
Kampaundi za kalisi ni pia msingi wa saruji na hivyo wa ujenzi wa kisasa. Chokaa ni kiungo cha lazima wakati wa kutengeneza feleji.
Salfati ya kalisi (Ca[SO4] • 2 H2O) ni jasi.
-
Kalisi tupu ikitunzwa katika gesi ya arigoni ndani ya chupa
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kalisi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |