[go: up one dir, main page]


Arigoni (pia: argoni, ing. Argon, kut. kigiriki ἀργό(ν) „mvivu“ kwa sababu haipende kumenyuka kikemia) ni elementi yenye namba atomia 18 na uzani wa atomi 39.948. Alama yake ni Ar.

Arigoni
Jina la Elementi Arigoni
Alama Ar
Namba atomia 18
Mfululizo safu Gesi adimu
Uzani atomia 39.948
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 83.80 K (−189.35 °C)
Kiwango cha kuchemka 87.30 K (−185.85 °C)
Kiwango utatu 83.8058 K
Asilimia za ganda la dunia 4 · 10-4 %
Hali maada gesi
Mengineyo {{{mengineyo}}}

Duniani yapatikana katika angahewa kama gesi adimu na bwete isiyo na rangi wala ladha. Kwa sababu ya tabia yake ya ubwete kampaundi asilia hazijulikani ila tu zimetengenezwa katika maabara. Katika angahewa ni gesi adimu inayopatikana kwa wingi kwa sababu asilimia moja ya hewa yote ni arigoni.

Inapatikana wakati wa kupoza hewa kwa shabaha ya kupata oksijeni au hidrojeni ya kiowevu.

Kutokana ubwete wake hutumiwa kama gesi ya kuzuia mmenyuko kwa mfano katika vizima moto au ndani ya balbu inapochelewesha kuchomwa kwa nyuzi za balbu.