[go: up one dir, main page]

Uchapakazi Quotes

Quotes tagged as "uchapakazi" Showing 1-5 of 5
Enock Maregesi
“Mbegu tunazopanda leo ni mazao ya msimu ujao. Ukipanda mbegu mbaya utavuna mabaya. Ukipanda mbegu nzuri utavuna mazuri. Ukitenda mabaya leo kesho yako itakuwa mbaya. Ukitenda mazuri leo kesho yako itakuwa nzuri. Okoa kesho leo kwa kupanda mbegu nzuri na kuzimwagilia kwa imani na upendo kwa watu. Mungu ataleta mvua, jua na ustawi wa mazao yako. Panda mbegu ya msamaha kwa maadui zako, uvumilivu kwa wapinzani wako, tabasamu kwa marafiki zako, mfano bora kwa watoto wako, uchapakazi kwa kazi zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, ndoto kwa malengo yako, na uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli. Kila mbegu irutubishwe kwa mapenzi huru yasiyokuwa na masharti yoyote, au mapenzi huru yasiyokuwa na unafiki wa aina yoyote ile. Usifiche vipaji vyako. Ukiwa kimya utasahaulika. Usipopiga hatua utarudi nyuma. Usiwe na hasira, wivu au ubinafsi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hasanati ni matendo mema. Mema yanatoka kwa Mungu. Mabaya yanatoka kwa Shetani. Mke mwema anatoka kwa Mungu. Mke mbaya anatoka kwa Shetani. Mke mwema ana hekima na busara, ana maadili na tabia njema, ana utu na uchapakazi, ana wema na upendo, na ana aibu kwa wanaume.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Radia hakuwa na makosa. Wengi huishi maisha yao bure. Yeye aliishi ya kwake kwa ajili ya watu. Hakuishi tu kama raia wa Tunisia. Aliishi kama raia wa uanadamu, maadili mema na uchapakazi. Watu walimsifu kwa kuwa na kaulimbiu ya 'Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta'.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. 2 + 2 = 5. Umoja una sisi (ubinadamu), si mimi (ubinafsi). Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano watakuwa na nguvu ya watu watano! Watakuwa na nguvu ya ziada kufanikisha malengo kama vile kuwa na uwezo wa kusaidia jamii kama timu au kama mtu binafsi, kujenga jengo la ofisi, kutengeneza ziada katika masuala ya uchumi wa kampuni au nchi au wa mtu binafsi, ushindi katika kitu chochote kile, na kadhalika. Mimi ni ubinafsi. Sisi ni ubinadamu. Ubinafsi ni uvivu. Ubinadamu ni uchapakazi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna siri nyingi za ndani zinazofanya mtu aendelee kufanikiwa, na kuna siri nyingi za nje zinazofanya mtu aendelee kuficha siri ya mafanikio yake. Siri za ndani ni siri za kweli, ilhali siri za nje ni siri za uongo, zenye lengo la kuficha ukweli. Hata hivyo, siri ya mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii na maarifa, pamoja na siri.”
Enock Maregesi