[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Uwezo wa kusoma na kuandika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Upatikanaji wa uwezo wa kusoma na kuandika (literacy rate) katika nchi za dunia.
Bili ya uuzaji wa mtumwa wa kiume na wa jengo huko Shuruppak, iliyoandikwa kwa Kisumeri mnamo 2600 KK.

Uwezo wa kusoma na kuandika (kwa Kiingereza: literacy) ni elimu muhimu katika jamii za kisasa.

Katika jamii za kijadi mawasiliano kati ya watu yalitokea hasa kwa njia ya kimdomo au njia nyingine za kuelewana uso kwa uso.

Lakini tangu kutokea kwa madola yanayounganisha watu wengi katika eneo kubwa habari muhimu huhifadhiwa kwa njia ya maandishi. Uwezo wa kusoma na kuandika umekuwa msingi kwa kushiriki kikamilifu katika jamii za aina hii.

Kwa kawaida watu hujifunza kusoma na kuandika katika shule.

Tamko la shirika la UNESCO lasema: “Kujua kusoma na kuandika ni haki ya kila mtu, jambo hilo linasaidia mtu kuwa na uwezo, na ni njia ya kumwezesha kupata maendeleo katika maisha yake binafsi na pamoja na watu wengine.”

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]