[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Sosholojia ya elimu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sosholojia ya elimu ni sayansi inayohusu uhusiano ya elimu na jamii.

Kwa upana zaidi, elimu ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa kimaksudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.

Walimu katika taasisi za elimu huratibisha elimu ya wanafunzi wao kupitia masomo kama vile ya kuandika, kusoma, hesabu, sayansi na historia. Mbinu hii wakati mwingine huitwa masomo haswa tunaporejelea somo la aina fulani, kwa kawaida mbinu hii hutumiwa na maprofesa katika taasisi za masomo ya juu. Kuna elimu maalum kwa wale wanaohitaji ujuzi wa kitaaluma, kama vile wale wanaohitaji kuwa marubani. Juu ya hayo, kuna nafasi nyingi za elimu katika viwango vingine visivyo rasmi kama vile majumba ya ukumbusho, maktaba pamoja na mtandao na tajriba za maisha.

Haki ya kusoma imeweza kuelezwa kuwa haki ya kimsimgi ya binadamu katika kifungu cha pili cha itifaki ya kwanza ya Maagano ya haki za binadamu barani Ulaya kuanzia mwaka wa 1952 ambapo wanachama wote wanashurutishwa kuhakikisha elimu kwa wote. Katika kiwango cha kimataifa, Mapatano ya Umoja wa Mataifa ya haki za kiuchumi, kijamii na utamaduni katika mwaka wa 1966 yanahakikisha haki hii katika kifungu cha 13.

Mifumo ya elimu rasmi

[hariri | hariri chanzo]

Elimu ni dhana inayorejelea namna ambayo wanafunzi wanaweza kujifunza kitu:

   Mwongozo unarejelea urahisishaji wa somo na hulenga kutambua shabaha zilizobuniwa na mwalimu au mbinu zingine za kufunza.
   Kufunza kunarejelea matendo halisi ya mwalimu yanayonuia kupasha elimu kwa wanafunzi.
   Kujifunza hurejelea masomo yenye mtazamo unaolenga kuwapa wanafunzi elimu, ujuzi na uwezo unaoweza kutumika punde tu wakamilishapo kipindi cha masomo.

Elimu Ya Msingi

[hariri | hariri chanzo]
   Makala kuu ya: Primary education
   Shule ya msingi ya wazi hewa. Mwalimu (kuhani) na darasa kutoka nje ya jiji la Bukarest, karibu 1842.
   Masomo ya msingi huchukua kati ya miaka 5-7 ya kwanza ya elimu rasmi. Kwa jumla elimu ya juu hujumulisha miaka 6-8 ya masomo kuanzia mwaka wa tano au sita, lakini hutofautiana baina na kati ya nchi. Asilimia 70 ya watoto waliotimu umri wa kujiunga na shule hujiandikisha katika masomo ya msingi kote ulimwenguni na viwango hivi vinaongezeka.[1] Chini ya Elimu kwa mipango yote inaendeshwa na UNESCO, nchi nyingi wana nia ya kufanikisha zima uandikishaji katika elimu ya msingi ifikapo mwaka 2015, na katika nchi nyingi, ni lazima kwa watoto kupata elimu ya msingi.Chini ya mpango wa elimu kwa wote ulioanzishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja Wa Mataifa (UNESCO), nchi nyingi zimejitole

Elimu Ya Shule za Upili

[hariri | hariri chanzo]
   Makala kuu ya: Secondary education

Katika mifumo ya kisasa ya elimu ulimwenguni, elimu ya shule za upili au sekondari huchukua kipindi cha pili cha elimu rasmi ambayo hutokea wakati wa ujana wa wanafunzi.[onesha uthibitisho] Mfumo huu hutambulika kutoka kwa masomo ya msingi ambayo ni ya lazima, ni ya jumla na yanayofanana. Yale ya shule za upili ni teule na ya hiari.[onesha uthibitisho] Shule hizi hujulikana kama sekondari, shule za upili, shule za wastani, vyuo au shule za ujuzi wa kitaalamu kulingana na kipindi au mfumo unaofuatwa. Maana ya dhana hizi hutofautiana kutoka mfumo mmoja hadi mwingine. Mpaka kamili kati ya elimu ya msingi na ya upili hutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine, tofauti hizi zipo hata katika nchi lakini kwa kijumla hutokea kati ya mwaka wa saba na wa kumi wa kusoma. Elimu ya sekondari hutokea katika umri wa ujana. Nchini Marekani na Kanada, elimu ya msingi na sekondari kwa pamoja hurejelewa kama elimu ya K-12 na katika nchini ya Nyuzilandi, elimu hii hurejelewa kama elimu ya miaka 1-13. Azma ya elimu ya sekondari ni kutoa maarifa ya kawaida, kutayarisha wanafunzi kwa elimu ya juu au kuwafunza watu kazi moja kwa moja.

Elimu ya sekondari iliibuka nchini Marekani mwaka wa 1910 na ilisababishwa na kuwepo kwa biashara kubwa na maendeleo ya kiteknolojia viwandani. Ili kuafikia mahitaji ya kazi, shule za upili zilijengwa na mtaala uliolenga maarifa ya kazi za ofisi na za sulubu ukazinduliwa. Hii ilibainika kuwa njia ya manufaa kwa mwajiri kwani uimarishaji wa huduma za kibinadamu uliwafanya waajiriwa kuwa madhubuti kazini na kushusha gharama kwa waajiri huku waajiriwa wakinufaika na mishahara minono ikilinganishwa na waliokuwa na elimu ya msingi pekee.

Barani Ulaya, shule za sarufi au akademia zilikuwepo hata katika miaka ya 1500. Shule za umma au zile za kulipa karo au hata shule za ufadhili na wakfu zina historia ndefu zaidi.

Elimu ya juu

[hariri | hariri chanzo]
   Makala kuu ya: Higher education

Chuo Kikuu cha Cambridge ni taasisi za elimu ya juu.

Elimu ya juu, yaani ile ya baada ya shule ya upili au elimu ya awamu ya tatu, si ya lazima. Elimu hii kwa kawaida hujumulisha viwango vya shahada ya kwanza, ya uzamili, ya uzamifu pamoja na elimu ya ujuzi wa kitaalamu. Kwa jumla elimu ya juu hutolewa na vyuo na vyuo vikuu. Kwa jumla elimu ya juu hutolewa na vyuo na vyuo vikuu. Elimu ya juu huambatana na kutolewa kwa vyeti, stashahda za diploma na shahada za digrii kitaaluma.

Masomo ya viwango vya juu hujumuisha elimu, utafiti na huduma za jamii na katika uwanja wa elimu, hujumulisha viwango vya shahada ya kwanza na nyingine za juu. Elimu ya juu aghalabu huhusu kufuzu katika kiwango cha shahada ya kwanza.[[]] kufuzu. Idadi kubwa ya watu katika nchi zinazoendelea (hadi kufikia asilimia 50%) wameweza kupata elimu ya juu wakati fulani maishani mwao. kwa hivyo, elimu ya juu ni muhimu kwa uchumi wa taifa, ni kiwanda cha pekee ambacho huzalisha wafanyikazi walioelimika.[onesha uthibitisho]

Elimu Ya Ngumbaru

[hariri | hariri chanzo]
   Makala kuu ya: Adult education

Elimu ya ngumbaru au ya watu wazima imekuwa kawaida katika nchi nyingi. Elimu hii huchukua maumbo mengi yakiwemo elimu rasmi darasani, elimu ya kibinafsi na masomo ya mtandao. Idadi fulani ya kozi za kazi maalum kama vile elimu kuhusu mifugo, maswala ya madawa, maswala ya uwekezaji, uhasibu na kozi zinginezo kwa sasa hupatikana mtandaoni.

Elimu Badala

[hariri | hariri chanzo]
   Makala kuu ya: Alternative education

Elimu badala, ambayo pia hujulikana kama elimu, isiyo ya kidesturi , ni dhana yenye maana pana na inayoweza kutumiwa kurejelea aina zote za elimu zilizo nje ya elimu ya kidesturi (kwa watu wote na viwango vyote vya elimu). Hujumuisha sio tu mitindo ya elimu inayokusudiwa wanafunzi wenye mahitaji ya kipekee lakini pia mitindo inayolenga hadhira ya jumla na kutumia mitindo na falsafa badala ya elimu.


Elimu badala mara nyingi huwa ni matokeo ya mabadiliko katika elimu yaliyotokea katika misingi mbalimbali ya falsafa ambayo kwa kawaida ni tofauti na elimu ya kijadi ya lazima. Mabadiliko mengine yana misingi ya kisasa, kiutafiti au kifalsafa, ilhali mengine ni miungano isiyo rasmi kati ya walimu na wanafunzi wasioridhika na maswala fulani ya elimu hiyo ya kijadi.[onesha uthibitisho] Elimu badala hii ambayo ni pamoja na shule za tabia, shule za badala, shule zinazojitegemea na masomo ya nyumbani hutofautiana pakubwa kivyao, lakini zote hutilia maanani umuhimu wa idadi ndogo ya wanafunzi darasani na mahusiano ya karibu kati ya wanafunzi na walimu vilevile husababisha hali ya umoja.[onesha uthibitisho] .

Elimu ya asili

[hariri | hariri chanzo]

Kuongezwa kwa ruwaza za elimu ya asili (mbinu na maudhui yake) ndani ya elimu badala katika eneo la mfumo wa elimu rasmi na elimu isiyo rasmi kumewakilisha kipengele muhimu kilichochangia ufanisi wa mfumo wa elimu asili kwa wanajamii asili walioamua kufuata njia hii; hii ikiwa ni pamoja na wanafunzi na walimu.

Kuingizwa kwa mbinu za asili kama vile kujua, kusoma, kuelekeza, kufunza na kusoma kama njia nzuri ya kuhakikisha kuwa wanafunzi/wanagenzi na walimu/waelekezi wanaweza kufaidika kutokana na elimu kwa njia ya kiasili iliyokuza, kutumia na kuendeleaza uhamasishaji wa tamaduni za kiasili.[2]

Kwa wanafunzi au wagenzi na walimu au waelekezi, kuwekwa pamoja kwa mbinu hizi mara nyingi huongeza fanaka, matarajio na matokeo ya elimu. Hili huafikiwa kwa kutoa elimu inayooana na taswira zao za asili, mazoea na mitiazamo yao ya ulimwengu. Kwa wanafunzi na walimu wasio wa asili, elimu ya aina hii ina athari ya kuongeza ufahamu wa tamaduni zao za kibinafsi na mazoea ya jumla ya umma na watu wanaowazunguka, hivyo basi kukuza heshima na kuthamini tamaduni za wanajamii hizo.

Katika elimu na mafunzo, kujumuishwa kwa maarifa ya kiasili, tamaduni, maono, mitazamo na dhana katika mitaala, vifaa vya kuelekeza na vitabu vya kozi vina athari kubwa kama ile ya kujumuisha mbinu za asili katika elimu ambayo hunufaisha walimu na wanafunzi katika usambamba wa masomo, kufaulu na matokeo ya masomo hayo. Ambayo hunufaisha walimu na wanafunzi katika usambamba wa masomo, kufaulu na matokeo ya masomo hayo. Walimu na wanafunzi wa kisasa wana heshima, hamasa na maridhio kwa jamii na watu wa kienyeji kutokana na elimu husishi wanayopata.[3]

Mfano mkuu unaoonyesha mbinu na maudhui ya asili yanaweza kukuza matokeo yaliyotajwa hapo juu undhihirika katika elimu ya juu nchini Kanada. Kwa sababu ya sheria fulani, dhamira ya kuongeza mafanikio kwa wanafunzi wa elimu asili na kukuza maadili ya jamii ya kitamanduni, kuingizwa kwa mbinu na maudhui ya asili katika elimu huonwa kuwa jukumu na wajibu wa serikali na taasisi za elimu zenye mamlaka.[4]

Mchakato

[hariri | hariri chanzo]
   Makala kuu yas: Curriculum and List of academic disciplines

Somo la taaluma ni tawi la elimu ambalo hufunzwa kirasmi katika vyuo vikuu ama kupitia njia zingine kama hizo. Kwa kawaida, kila somo huwa na masomo mengine ama matawi na mipaka ya kuyabainisha mara nyingi huwa si dhahiri na na mara nyingine husababisha utata. Mifano ya masomo ya kitaaluma yenye upana ni kama vile sayansi asilia, hesabu, sayansi ya komputa, sayansi za jamii, sayansi za binadamu na sayansi za matumizi.[5]

Mitindo ya kujifunza

[hariri | hariri chanzo]

Kuna utafiti uliofanyawa kuhusu mitindo ya kusoma katika miongo miwili iliyopita. Dunn na Dunn [6] walilenga kutambua vichangamshi husishi vinavyofanya masomo yavutie na namna ya kutawala mazingira ya shule, baadaye Joseph Renzuli [7] alipendekeza mikikati tofautitofauti ya kufunza. Howard Gardner[8] alitambua talanta ama vipaji vya mtu binafsi katika nadharia zake za akili nyingi. Kwa misingi ya kazi za Jung “Kielezi Aina cha Myers Briggs” na “kitenga tabia cha Keisresy” [9]vililenga kuelewa jinsi nafsi za watu huathiri uhusiano wa mtu binafsi na zinavyoathiri maelewano ya watu katika mazingira ya kujifunza. Kazi za David Kolib na Anthony Gregorc “jinsi ya kusawiri”[10] ” hufuata mfano kama huu lakini uliorahisishwa.

Kwa wakati huu, kugawika kwa elimu katika mitindo tofautitofauti hukubalika na wengi. Huenda ikawa kuwa mitindo[11] ya kujifunza ndiyo ya kawaida:[12]

   Kuona: Masomo yenye misingi ya kutazama kwa makini na kuona kile kinachosomwa.
   Kusikiza: Kusoma kwa misingi ya kusikiliza maelezo/habari.
   Masomo husishi: Kusoma kwa misingi ya kutumia mikono na vitendo husishi.

Imedaiwa kuwa kulingana na mtindo wa kujifunza unaopendelewa, mbinu tofautitofauti za kufunza huwa na matokeo ya viwango tofauti.[13] Umuhimu wa nadharia hii ni kuwa kunakofaa, inapaswa kutumia mbinu mbalimbali za kufunza zinazojumulisha mitindo yote mitatu ya kufunza ili wanafunzi tofautitofauti wapate fursa ya kujifunza kwa njia inayowafaa.[14] Guy Claxton ametilia shaka mitindo ya kujifunza kama vile VAK kwani kwa kiasi fulani mitindo hii ina mazoea ya kupachika watoto majina hivyo basi kuwazuia kujifunza.[15]

Kujifunza

[hariri | hariri chanzo]

Walimu wanapaswa kuelewa somo vilivyo ilikuwasilisha umuhimu wake kwa wanafunzi. Shabaha hapa ni kuunda misingi ya ujuzi kamili ambayo wanafunzi wanaweza kutumia kujijenga zaidi kwani wamewekwa wazi kwa matukio mbalimbali ya maisha. Walimu wazuri huweza kutafsiri habari kama hukadiria vizuri, hutumia mazoea na hekima hadi kwa elimu husika ambayo mwanafunzi anaweza kuelewa, kuhifadhi na kupititishia wengine. Utafiti kutoka Marekani unatoa maoni kuwa ubora wa walimu ndio kigezo kinachoathiri mafanikio ya wanafunzi, na kuwa nchi zinazopata alama za juu katika mtihani au majaribio ya kimataifa zimeweka sera chungu nzima zinazohakikisha kuwa walimu wanaoajiri ndio bora. [16]

Teknolojia

[hariri | hariri chanzo]
   Makala kuu ya: Educational technology

Teknolojia ni kigezo muhimu katika elimu. Tarakilishi na simu za rununu zinatumiwa katika nchi zilizoendelea kuimarisha elimu iliyothibitishwa na kukuza njia mpya za elimu kama vile elimu ya mtandao (masomo ya mbali). Wanafunzi hupata fursa ya kuchagua wanachotaka kusoma. Kuenea kwa tarakilishi pia kunamaanisha kuongezeka kwa programu za komputa na kuongeza habari mtandaoni. Teknolojia hutoa vifaa muhimu vinavohitaji ujuzi mpya na uelewa wa wanafunzi zikiwemo njia nyingi za mawasiliano, na huleta njia mpya za kuhusisha wanafunzi kama vile mazingira ya kujifunza. Teknolojia inatumiwa sio tu katika wajibu wa kutawala katika elimu bali pia katika kuwaelekeza wanafunzi. Matumizi ya teknolojia kama vile virusha maandishi (power point) na ubao mweupe hutumiwa kunasa akili za wanafunzi darasani. Teknolojia vilevile hutumiwa kuwatahini wanafunzi. Mfano mzuri ni mfumo wa kuvutia hadhira (ARS),ambao huruhusu majibu ya mitihani moja kwa moja pamoja na majadiliano darasani.

Teknolojia za habari na mawasiliano (ICT) ni "seti ya vifaa na rasilimali mbalimbali zinazotumiwa kuwasiliana, kuunda, kueneza na kuongoza habari."[17] Teknolojia hizi ni pamoja na kompyuta, mtandao, teknolojia za kusambaza habari (redio na televisheni) na simu. Kuna mvuto unaoongezeka kuhusu namna tarakilishi na mtandao zinavyoweza kuimarisha elimu katika viwango vyote, yaani mseto wa elimu rasmi na ile isiyo rasmi.[18] Teknolojia za habari na mawasiliano za awali, kama vile redio na televisheni, zimetumiwa kwa zaidi ya miaka 40 kwa elimu wazi na ile ya mbali, hata hivyo kupiga chapa ndiyo njia nafuu zaidi, inapatikana kwa urahisi, na hivyo basi ni mbinu iliyotawala katika nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea.[19]

Matumizi ya tarakilishi na mtandao bado ni changa (ikiwa vinatumika) katika nchi zinazoendelea, na hii ni kwa sababu miundo msingi ni michache na ghali. Kwa kawaida teknolojia kadhaa hutumiwa kwa pamoja bali siyo mbinu moja pekee ya kupokelewa. Kwa mfano, Kothmel Community Radio Internet hutumia matangazo ya redio na kompyuta pamoja na teknolojia ya mtandao, na hivyo hurahisisha kugawa habari na kutoa nafasi za elimu katika kijiji fulani kule Sri Lanka.[20] Chuo kikuu cha Uingereza (UKOU) kilichoanzishwa mwaka wa 1969 kama taasisi ya elimu ya kwanza ulimwenguni kujitolea kutoa elimu ya wazi na ya mbali, bado hutegemea vifaa vilivyopigwa chapa na kuongezea redio, runinga na hivi majuzi programu zilizounganishwa na kompyuta.[21] Vivyo hivyo, Chuo Kikuu cha Indira Gandhi nchini India huweka pamoja matumizi ya chapa, sauti zilizorekodiwa, video, redio, televisheni na teknolojia ya vielezo vya kusikiza mkutano.[22]

Dhana ya “masomo yanayosaidiwa kwa Kompyuta” (CAL) limetumiwa kwa wingi kuelezea teknolojia katika masomo.

Nadharia ya elimu

[hariri | hariri chanzo]
   Makala kuu ya: Education theory

Nadharia ya elimu ni nadharia ya azma, mataumizi na ufafanuzi wa elimu na kusoma. Historia yake inatokana na wataalamu wa elimu kutoka Ugiriki kuanzia karne ya 18. Katika karne ya 20 mbinu za kusoma zimetumia nadharia katika kufunza, kutathmini na katika sheria za elimu ambazo hupatikana katika vitengo mbalimbali kama ifuatavyo:

   Makala kuu ya: Economics of education

Sababu zimetolewa kuwa kiasi cha juu cha elimu ni muhimu kwa nchi kwa ajili ya kuwezesha ukuaji haraka wa uchumi.[23] Uchunguzi unaotegemea nadharia huunga mkono nadharia za kutabiri kuwa nchi masikini zinapaswa kukua haraka kuliko nchi tajiri kwani nchi hizi zinaweza kutumia teknolojia mpya kabisa ambayo imeshajaribiwa na nchi tajiri. Hata hivyo, kuhamisha teknolojia kunahitaji viongozi wenye maarifa na wahandisi wenye uwezo wa kutumia mashine mpya ama mazoezi ya uzalishaji yaliyokopwa ili kuziba mpaka kwa miigo. Hivyo basi, uwezo wa nchi wa kujifunza kutoka kwa nchi kiongozi ni jukumu la wafanyakazi wa nchi hiyo.[24] Utafiti wa hivi karibuni wa vitambulishi vya kujumuisha ukuaji wa kiuchumi umesisitiza umuhimu wa vyuo asili vya uchumi[25] na majukumu ya ujuzi tambuzi.[26]

Katika kiwango cha mtu binafsi, kuna maandishi yenye uhusiano na kazi ya Jacob Mincer, [27] ya jinsi mapato yanahusiana na elimu na rasilimali ya mtu binafsi. Kazi hii imetia motisha idadi kubwa ya utafiti lakini pia inaelekea kuleta mabishano kwa kiasi fulani. Ubishi mkubwa unazunguka jinsi ya kufasiri matokeo ya kusoma.[28]

Wataalam wa uchumi Samwel Bowels na Herbert Ginits walitoa maoni kwamba kulikuwa na ubishi asili katika elimu nchini Marekani kati ya shabaha ya kidemokrasia shirikishi yenye usawa na faida ya mapato ya kikapitolisti yaliyodokeza hali ya kutokuwa na usawa.[29]

Historia

[hariri | hariri chanzo]
   Makala kuu ya: History of education

A depiction wa Chuo Kikuu cha Bologna, Italia

Historia ya elimu kulingana na Dieter Lenzen rais wa Freie Universitat Berlin mwaka wa 1994, "ilianza miaka mingi iliyopita ama mwishoni wa mwaka wa 1770". Elimu kama sayansi haiwezi kutengwa na tamaduni za elimu iliyokuwepo awali. Wakubwa waliwafunza wadogo wao juu ya jamii kwa kutumia maarifa na ujuzi waliohitaji kufahamu na mwishowe kupitisha.[onesha uthibitisho] Mabadiliko ya tamaduni na binadamu kama spishi kulitegemea mazoea ya kupitisha elimu.[onesha uthibitisho] Katika jamii ambazo hazikujua kusoma, hili liliafikiwa kupitia kwa mdomo na kuiga. Kusimuliana hadithi kuliendelezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Lugha ya mazungumzo iliendelea na kuwa ishara na herufi. Kina na upana wa elimu au maarifa ulioweza kuhifadhiwa na kupitishwa uliongezeka zaidi.[onesha uthibitisho] Wakati ambapo tamaduni zilianza kupanua elimu zaidi ya ujuzi wa kawaida wa mawasiliano, biashara, kukusanya chakula, desturi za kidini na kadhalika, elimu rasmi na kupata kisomo mwishowe kulifuatia.[onesha uthibitisho] Kisomo kwa maana hii kilikuwa kimeshaanza nchini Misri kati ya 3000 na 500 Kabla Kristo (BC).[onesha uthibitisho]

Siku hizi aina fulani ya elimu ni jambo la lazima kwa watu wote katika nchi nyingi. Kwa sababu ya ongozeko la watu na kuenea kwa elimu ya lazima, Shirika La Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limepiga hesabu ya kwamba miaka 30 ijayo, watu wengi zaidi watapata elimu rasmi katika historia ya binadamu ulimwenguni.[30]

   Makala kuu ya: Philosophy of education

John Locke kazi Baadhi ya Mawazo Kuhusu Elimu ilikuwa imeandikwa katika 1693 na bado elimu ya jadi huonyesha vipaumbele katika dunia ya Magharibi

Falsafa ya elimu ni utafiti wa kifalsafa juu ya kusudi, utaratibu na ubora wa elimu. Falsafa ya elimu kwa kawaida huonwa kama tawi la falsafa na elimu. Falsafa ya elimu mara nyingi huhifadhiwa ndani ya falsafa na elimu ilhali ni falsafa matumizi, iliyotokana na nyanja za zamani za falsafa (ontolojia,elimu adili, epistemolojia) na njia (kisia, taswira na tafiti) mbinu na mtaala, nadharia, kwa kutaja tu chache.

Saikolojia

[hariri | hariri chanzo]
   Makala kuu ya: Educational psychology

A darasa kawaida majaribio katika fann Marekani kuhudhuria madarasa ndogo kwa miaka 3 au zaidi katika darasa mapema iliongezeka high shule viwango vya kuhitimu wanafunzi kutoka familia zenye kipato cha chini. [31]

Saikolojia ya elimu ni uchunguzi wa jinsi watu hujifunzi katika mandhari ya elimu, ufaafu wa maingiliano ya elimu, saikoloji ya kufunza na saikolojia jamii za shule. Ingawa maneno “saikolojia ya kielimu” na “saikolojia ya shule“ mara nyingi hutumiwa kwa kubadilishana, watafiti na wananadharia wanaweza kutambuliwa kama wanasaikolojia wa elimu, ilhali weledi wanaopatikana shuleni au mandhari yanayaoana na shule hujulikana kama wanasaikolojia wa shule.[onesha uthibitisho] Saikolojia ya elimu inajishughulisha na utaratibu wa kutoa elimu kwa watu na umma kwa jumla na umma mdogo, kama vile watoto wenye vipaji na wale wenye ulemavu maalum.[onesha uthibitisho]

Saikolojia ya elimu inaweza kueleweka kwa sehemu kupitia masomo mengine. Saikolojia ya elimu vilevile huarifiwa na saikolojia, ikileta uhusiano baina ya utabibu na bayolojia.[onesha uthibitisho] . Saikolojia ya elimu pia huarifu masafa mapana ya masomo maalum yakiwemo mpango wa mafunzo.[onesha uthibitisho] Teknolojia ya elimu, mtaala uliokuzwa, masomo yaliyopangwa, masomo maalum, sayansi tambuzi na sayansi masomo.[onesha uthibitisho] Katika vyuo vikuu, idara za elimu ya saikolojia vimehifadhiwa katika vitivo vya elimu. Hii ni kwa sababu ya uwezekano wa ukosefu wa uwakilishaji wa maudhui ya saikolojia ya elimu katika utangulizi wa vitabu vya saikolojia.

Sosholojia

[hariri | hariri chanzo]
   Makala kuu ya: Sociology of education

Sosholojia ya elimu ni somo linalohusu jinsi taasisi za kijamii na kani huathiri michakato na matokeo ya elimu, na kinyume chake. Kwa wengi, elimu hueleweka kama mbinu ya kushinda vizuizi, kufanikisha usawa na kupata amani na hadhi kwa wote (Sargent 1994). Wanafunzi wanaweza kutiwa motisha na tamaa ya maendeleo na uboreshaji. Elimu hutambuliwa kama mahali ambapo watoto huweza kujikuza kulingana na mahitaji yao ya kipekee.[32] Jukumu la elimu laweza kuwa ni kukuza mtu binafsi hadi kilele.[onesha uthibitisho] Uelewa wa shabaha na mbinu za michakato ya utangamano wa kielimu hutofautiana kulingana na dhana ya sosholojia iliyotumika.

Maendeleo ya Kielimu

[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya dunia ikionyesha Elimu Index (kulingana na Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2007/2008)

Katika nchi zinazoendelea idadi na uzito wa shida zilizoko kwa kawaida ni kubwa.[onesha uthibitisho] Watu wa vijijini wakati mwingine huwa hawana habari kuhusu umuhimu wa elimu. Hata hivyo, nchi zingine zina wizara ya elimu na katika masomo mengi kama vile kujifunza lugha za kigeni, kiwango cha elimu kimo juu zaidi kuliko ilivyo katika nchi zilizoendelea. Kwa mfano, ni kawaida kupata wanafunzi katika nchi zinazoendelea wakizungumza lugha nyingi za kigeni kwa usanifu mkubwa ilhali jambo hili ni nadra katika nchi zilizoendelea ambapo idadi kubwa ya watu huzungumza lugha moja.

Vilevile kuna shinikizo la kiuchumi kutoka kwa wazazi ambao hupendelea watoto wao wapate pesa kwa muda mfupi kuliko faida za elimu ya muda mrefu.[onesha uthibitisho] Utafiti wa hivi karibuni kuhusu ajira ya watoto na umasikini zimependekeza kuwa familia zilizokumbwa na umasikini zinapofikia kiwango fulani cha kukidhi mahitaji yao ya kimsingi, wazazi huwarejesha watoto wao shuleni.[onesha uthibitisho] Hii imethibitshwa kuwa kweli mara tu kizingiti kinapovukwa. Hata kama uwezekano wa thamani ya kiuchumi ya ajira ya watoto inaongezeka baada yao kurudishwa shuleni.[onesha uthibitisho] Urusi ina zaidi wahitimu kielimu kuliko nchi nyingine yoyote katika Ulaya.

Ukosefu wa vyuo vikuu bora na kiwango cha chini cha kukubalika katika vyuo hivi ni dhahiri katika nchi zilizo na idadi kubwa ya watu.[onesha uthibitisho] Baadhi za nchi zina mitaala mikuu inayoweza kubadilika kwa urahisi, inayofanana na yenye miundo zaidi.

   Kutokana na utandawazi shinikizo kwa wanafunzi katika shughuli za mtaala zimeongezeka
   Kuondolewa kwa asili mia fulani ya wanfunzi kwa ajili ya uboreshaji wa masomo (kwa kawaida hufanywa shuleni baada ya daraja la kumi)

India inakuza teknolojia na mtandao. India ilizindua EDUSAT, elimu ya setilaiti ambayo inaweza kuwafikia wengi kwa gharama ya chini. Kuna pia mpango ulioanzishwa na shirika la OLPC, kundi lililotokana na maabara ya MIT lililoungwa mkono na mashirika makuu ili kukuza kompyuta ya kupakata ambayo ingeghalimu $100, ili kuwezesha kuwasilisha elimu ya programu ya kompyuta. Kompyuta hizi zimesambaa kote kufikia mwaka wa 2009. Kompyuta hizi zinauzwa au kutolewa kama msaada. Hii itawezesha nchi zinazoendelea kuwapa watoto wao elimu kwa kutumia mitambo.

Barani Afrika, shirika la NEPAD limezindua programu ya masomo ya mtandao inayotoa vifaa vya kompyuta na masomo ya mtandao kwa shule zote za msingi na upili kwa kipindi cha miaka kumi. Vikundi vya kibinafsi kama vile The Church Of Jesus Christ Of Latter Days Saints, wanajikakamua kuwapa watu fursa ya kupokea elimu katika nchi zinazoendelea kupitia miradi kama vile Perpetual Educational Fund. Mradi wa maendeleo kimataifa inayofahamika kama nabuur.com, com iliyoanza kutokana na usaidizi wa raisi wa Marekani Bill Clinton, hutumia mtandao kuwezesha ushirikiano wa watu binafsi kuzungumzia maswala ya maendeleo ya jamii.

Umataifishaji

[hariri | hariri chanzo]

Elimu inaendelea kuwa jambo la kimataifa. Sio vifaa vyake tu vinavyoendelea kuathiriwa na mazingira ya kimataifa yenye ukwasi bali pia mabadiliko ya wanafunzi katika viwango vyote yanayochangia kuendesha jukumu hili muhimu. Kwa mfano kule Uropa, programu ya Socratis Erusmus imechechemua mabadilishano kati ya vyuo vikuu vya Uropa. Vile vile, Shirika la Soros hutoa fursa nyingi kwa wanafunzi kutoka Asia ya kati na Uropa mashariki. Wasomi wengi hudai kwamba ingawa mfumo fulani unaweza kuzingatiwa kuwa bora au mbaya kuliko mwingine, kuzoea aina tofauti ya elimu mara nyingi huonwa kuwa elementi muhimu ya kuzoea masomo ya kimataifa.[33]

Dini na Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Tazama makala kuu: Elimu ya kidini

Elimu katika dini ya Uislamu ni muhimu kwa wake na waume[onesha uthibitisho], haswa kwa watoto wachanga. Kinyume na dhana ya kawaida[onesha uthibitisho], kutafuta aina zote za maarifa, yawe ya kitaaluma, kidini au ya dunia yanaruhusiwa kwa watu wa umri wowote. Hata hivyo, masomo ya umri mdogo huonwa kuipa akili fursa ya kumakinika bila kuathiriwa na shida na majukumu ya maisha ya utu uzima