Sakina Karchaoui
Sakina Karchaoui (alizaliwa 26 Januari 1996)ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Ufaransa ambaye anacheza kama beki wa kushoto wa klabu ya Division 1 Féminine Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Mzaliwa wa Salon-de-Provence, katika eneo la Provence nchini Ufaransa, Karchaoui alilelewa katika mji wa karibu wa Miramas na wazazi wake wa Morocco. Alianza kucheza mpira wa miguu katika mtaa wake na wavulana[1]. Baada ya miaka miwili katika klabu ya huko, US Miramas, alijiunga na Montpellier.[1]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Montpellier
[hariri | hariri chanzo]Karchaoui alipata mechi yake ya kwanza kwa Montpellier mnamo Novemba 2012 wakati wa ushindi wa 6-0 dhidi ya Vendenheim.[2] Katika msimu wa 2013-14 ,[3]Karchaoui aliichezea klabu hiyo mechi sita, na kufikisha jumla ya dakika 475 uwanjani.[3] Alichezea Montipellier kwanzia 2012 hadi 2020.
Lyon
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tarehe 24 Juni 2020, mabingwa watetezi wa ligi mara kumi na nne Lyon walitangaza kutia saini kwa Karchaoui kwa msimu wa 2020-21. [4]
Paris Saint-Germain
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tarehe 10 Julai 2021, mabingwa watetezi wa ligi Paris Saint-Germain walitangaza kumtia saini Karchaoui kwa mkataba wa miaka mitatu.[5]
Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Karchaoui aliitwa kwenye timu ya taifa ya wanawake kwa mara ya kwanza Aprili 2016. [6][7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Rising star Karchaoui seeking more days in the sun - FIFA.com". web.archive.org. 2016-11-14. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-11-14. Iliwekwa mnamo 2024-04-13.
{{cite web}}
: Cite has empty unknown parameter:|dead-url=
(help) - ↑ "France - S. Karchaoui - Profile with news, career statistics and history - Women Soccerway". us.women.soccerway.com. Iliwekwa mnamo 2024-04-13.
- ↑ 3.0 3.1 "France - S. Karchaoui - Profile with news, career statistics and history - Women Soccerway". us.women.soccerway.com. Iliwekwa mnamo 2024-04-13.
- ↑ "Montpellier HSC v Rodez 4–0". www.ol.fr. Iliwekwa mnamo 2024-04-13.
- ↑ NicolasB (2021-07-10). "Officiel - Karchaoui a signé au PSG jusqu'en 2024 !". ParisFans (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2024-04-13.
- ↑ http://www.footdelles.com/article/Equipe-de-France-A_Karchaoui-premiere-reussie_130271.html
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-10. Iliwekwa mnamo 2024-04-13.
{{cite web}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sakina Karchaoui kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |