[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Nusutropiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nusutropiki

Nusutropiki ni sehemu za dunia upande wa kusini na kaskazini ya kanda la tropiki. Yaeneo haya yako kwa jumla kati ya latitudo za 25° na 40° katika kila nusutufe ya dunia.-

Tabianchi ya subtropiki kwa jumla ni ya fufutende maana hakuna wala baridi kali wala joto kali sana. Hata hivyo miezi ya majirajoto inaweza kuwa na joto kubwa hasa pale ambako unyevuanga ni juu.

Wastani ya halijoto kwa mwaka wote ni juu ya 20 °C lakini wastani ya mwezi baridi zaidi ni chini ya 20 °C.