[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Mwanga wa Jua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanga wa jua ukiwa umezuiwa na mawingu.

Mwanga wa Jua (au nuru ya Jua; kwa Kiingereza sunlight au sunshine) ni mionzi kwa umbo la nuru inayoonekana, nuru ya infraredi na urujuanimno ambayo hutolewa na Jua. Mionzi hiyo ni sehemu za mnururisho wa sumakuumeme unaotoka kwenye Jua.

Kwenye Dunia, mwanga wa Jua huchujwa kupitia anga la Dunia na ni dhahiri kwamba mchana, wakati Jua lipo juu ya upeo wa macho, mionzi ya Jua inatufikia moja kwa moja kama mchanganyiko wa nuru ya kuangaza na kuleta joto. Wakati anga linafunikwa na mawingu, mwanga wa Jua unatawanyika.

Mwanga wa Jua huchukua muda wa dakika 8.3 kufikia Dunia kutoka kwenye uso wa Jua.

Upande wa afya mionzi ya Jua ina madhara lakini pia faida, kwa kuwa ni chanzo kikuu cha vitamini D3.

Tena mwanga wa Jua ni muhimu katika usanisinuru, mchakato unaotumiwa na mimea na viumbehai vingine vya jamii hiyo kubadili nishati ya mwanga, kuwa ndani ya nishati ya kemikali ambayo inaweza kutumika kwa kuchochea shughuli za viumbe.

Mwanga wa Jua huweza kupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Kipimajua (kwa Kiingereza: sunshine recorder, pyranometa).

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanga wa Jua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.