Mkoa wa Rukwa
Mkoa wa Rukwa |
|
Mahali pa Mkoa wa Rukwa katika Tanzania | |
Majiranukta: 7°0′S 31°30′E / 7.000°S 31.500°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | 4 |
Mji mkuu | Sumbawanga |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | Joachim Wangabo |
Eneo | |
- Jumla | 22,792 km² |
Idadi ya wakazi (2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 1,540,519 |
Tovuti: http://www.rukwa.go.tz/ |
Mkoa wa Rukwa ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 55000.
Unapakana na mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi upande wa kaskazini, mkoa wa Mbeya upande wa mashariki, Zambia kusini na upande wa magharibi Ziwa Tanganyika lililo mpaka na Kongo pia.
Makao makuu ya mkoa ni Sumbawanga.
Kabla ya kumegwa mwaka 2012 eneo la mkoa lilikuwa takriban km² 70,000. Kwa sasa lina kilomita ya mraba 22,792.
Kusini mwa mkoa liko ziwa Rukwa ambalo ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki.
Wilaya
[hariri | hariri chanzo]Wilaya ziko nne (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022 [1].):
- Sumbawanga Mjini (303,986)
- Wilaya ya Sumbawanga (494,330)
- Wilaya ya Nkasi (425,420)
- Wilaya ya Kalambo (316,783).
Wilaya ya Mpanda ilikuwa sehemu ya Rukwa ikawa kiini cha mkoa mpya wa Katavi kuanzia mwaka 2012.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa wakazi 139,019 [2], kwa asilimia kubwa waumini wa Kanisa Katoliki.
Kabila kubwa zaidi mkoani ndio Wafipa walioko hasa katika wilaya za Sumbawanga na Nkasi. Kati ya makabila mengine kuna Wamambwe-Lungu, Wawanda na Wanyamwanga katika wilaya ya Sumbawanga; kuna pia Wasukuma, Wanyamwezi na Wamasai.
Majimbo ya bunge
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Sumbawanga Mjini : mbunge ni Aeshi Hilaly (CCM)
- Nkansi Kaskazini : mbunge ni Anna Kenani (Chadema)
- Nkansi Kusini : mbunge ni Deuderit Mipata (CCM)
- Kwela : mbunge ni Deus Sangu (CCM)
- Kalambo : mbunge ni Kandege Sinkamba (CCM)
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti ya Mkoa wa Rukwa
- Matokeo ya sensa 2002: [1]
- Makabila na lugha za Tanzania: [2]
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Rukwa bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Rukwa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |