[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Machafuko ya Stonewall

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Machafuko ya Stonewall yalianza siku ya 28 Juni 1969 wakati polisi wa New York walipovamia Stonewall Inn, ambayo ni klabu ya mashoga katika mtaa wa Greenwich Village huko jimbo la New York. Polisi waliwatoa wafanyakazi na wateja nje ya baa hiyo, jambo ambalo lilisababisha maandamano ya siku sita na makabiliano makali na polisi nje ya baa hiyo na maeneo jirani. Uvamizi huo wa polisi ulisababisha machafuko miongoni mwa watu katika mtaa huo. Machafuko ya Stonewall yalikuwa kichocheo cha harakati za haki za mashoga nchini Marekani na duniani kote.

Stonewall Inn, 2016

Katika miaka ya 1950 na 1960, taasisi chache sana zilikaribisha mashoga. Taasisi ambazo ziliwakaribisha mashoga mara nyingi ziliendeshwa na vikundi vya uhalifu. Mara nyingi, wamiliki na wasimamizi wa baa hawakuwa mashoga. Mfumo wa kisheria unaochukia mashoga wa miaka ya 1950 na 1960 ulichochea makundi ya mashoga nchini Marekani kuthibitisha kwamba mashoga wanaweza kuingizwa katika jamii. Mwishoni mwa miaka ya 1960, kulikuwa na harakati nyingi za kijamii na kisiasa, ambazo ni pamoja na harakati la Haki za Kiraia na Harakati za Vita dhidi ya Vietnam. Harakati hizi zilitumika kama vichocheo vya Machafuko ya Stonewall.

Stonewall Inn

[hariri | hariri chanzo]

Stonewall Inn ni baa katika Greenwich Village, mtaa katika mji wa New York, ambayo ilikuwa mahali pa usalama kwa mashoga wa mji huu. Wakati huo, vitendo vya ushoga vilikuwa haramu katika kila jimbo isipokuwa Illinois, na baa na mikahawa inaweza kufungwa kwa kuwa na wafanyikazi au wateja mashoga. Kama vile baa na vilabu vingi vya mashoga, Stonewall Inn iliendeshwa na Mafia, ambao walihonga maafisa wa polisi kuwaacha.

Stonewall Inn ilikuwa taasisi muhimu ya Greenwich Village. Ilikuwa kubwa na ilikuwa na bei rahisi kuingia. Ilikaribisha "drag queens", ambao walipata sifa mbaya kwenye baa na vilabu vingine vya mashoga. Ilikuwa ni nyumba ya usiku kwa vijana mashoga wasio na makazi, ambao waliiba vitu dukani ili kumudu ada ya kuingia. Pia, ilikuwa moja ya baa chache za mashoga zilizobaki ambazo ziliruhusu kucheza dansi.

Machafuko

[hariri | hariri chanzo]

Polisi walivamia Stonewall Inn asubuhi ya 28 Juni 1969. Polisi waliingia ndani ya klabu, wakapigana na wateja, na wakapata pombe haramu. Walikamata watu 13, ikiwa ni pamoja na watu wanaokiuka sheria ya serikali ambayo unapaswa kuvaa nguo ambazo ni za jinsia yako. Wateja na wakaazi waliokuwa na hasira walikaa nje ya baa badala ya kuondoka kwa sababu walikuwa na hasira kuhusu unyanyasaji wa polisi na ubaguzi wa kijamii. Wakati mmoja, afisa mmoja alimpiga msagaji mmoja kichwani. Alipomlazimisha kuingia kwenye gari la polisi, alipiga kelele kwa watazamaji kuanza kuwarushia polisi senti, chupa, mawe na vitu vingine. Ndani ya dakika chache, machafuko kubwa na mamia ya watu ilianza. Polisi na watu wengine walijiweka kizuzi kwenye baa, ambayo umati huo ulijaribu kuichoma moto. Idara ya zima moto hatimaye iliweza kuzima moto, kuwaokoa waliokuwa ndani ya Stonewall, na kuwaondoa umati. Lakini maandamano hayo, yaliendelea katika eneo hilo kwa siku tano zaidi.

Ishara inayoonyesha kwamba Stonewall Inn ni ya kihistoria

Urithi wa Machafuko ya Stonewall

[hariri | hariri chanzo]

Katika kuadhimisha mwaka mmoja wa machafuko mnamo 28 Juni 1970, maelfu ya watu waliandamana katika mitaa ya Manhattan kutoka Stonewall Inn hadi Central Park. Iliitwa "Siku ya Ukombozi wa Mtaa wa Christopher," ambayo ilikuwa gwaride la kwanza la kujivunia la mashoga Amerika. Wimbo rasmi wa gwaride hilo ulikuwa: "Sema kwa sauti kubwa, mashoga anajivunia."

Mwaka wa 2016, Rais wa wakati huo Barack Obama aliteua eneo la machafuko kuwa ukumbusho wa kitaifa kwa kutambua msaada wa eneo hilo katika haki za mashoga.