Kiguudau
Mandhari
Kiguudau | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 3, spishi 3:
|
Viguudau ni ndege wa maji wa familia Heliornithidae. Familia hii ina spishi tatu tu, kila moja katika jenasi yake. Ndege hawa wana mwili mwembamba, shingo ndefu, mkia mpana na domo lenye ncha kali. Wana tando za ngozi kati ya vidole vyao zinazowasaidia kuogelea. Wanatokea kanda za tropiki kwa maji yatiririkayo polepole au katika vinamasi na mabwawa ya mikoko. Hula wadudu, makoa, gegereka, vyura na samaki wadogo. Hujenga tago lao la vitawi na mimea kwa matete.
Spishi ya Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Podica senegalensis, Kiguudau wa Afrika (African finfoot)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Heliopais personatus (Masked finfoot)
- Heliornis fulica (Sungrebe)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kiguudau wa Afrika
-
Masked finfoot
-
Sungrebe