[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kemia isiyokaboni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kemia isiyokaboni

Kemia isiyokaboni (au: Kemia isiyo ya kikaboni, pia kemia siogania; ing. inorganic chemistry) ni tawi la kemia linalochunguza yote ambayo si kemia kaboni yaani lisilotazama kampaundi za kaboni.

Kwa hiyo inaangalia michakato ya elementi zote isipokuwa kaboni na kampaundi zao yaani isiyo kampaundi ogania.

Asili ya kugawa kemia kwa matawi ya kemia kaboni na isiyo kaboni ilikuwa nia ya kutazama kwa pekee dutu zilizopatikana kiasili katika mazingira bila athira ya uhai pekee na dutu zinatokea na michakato ya viumbehai.

Kimsingi kuna tofauti kati ya

  • kemia chunganuzi (ing. analytical chemistry) inayouliza: Je kuna elementi na kampaundi gani katika dutu yoyote, na kwa viwano gani?
  • kemia sanisi (ing. synthetical chemistry) inayochunguza njia za kuunda dutiu mpya kwa kutengenezea kampaundi katika maabara au pia viwandani.


Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]