Jennifer Garner
Jennifer Garner | |
---|---|
Amezaliwa | Jennifer Anne Garner 17 Aprili 1972 |
Kazi yake | Mwigizaji |
Miaka ya kazi | 1995–hadi sasa |
Ndoa | Scott Foley (m. 2000–2003) (divorced) Ben Affleck (m. 2005–present) watoto wa 2 |
Jennifer Anne Affleck [1] (hasa hufahamika kwa jina lake la kuzaliwa kama Jennifer Garner; amezaliwa 17 Aprili 1972), ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Garner amejipatia umaarufu mkubwa kwa kucheza kwake kama kachero wa CIA, Sydney Bristow, katika kipindi cha mfululizo wa TV cha Alias, ambacho kilikuwa kikirushwa hewani na televisheni ya ABC kwa misimu mitano ambayo ilianza kuanzia 2001 hadi 2006. Wakati anafanyakazi kwenye Alias, amepata kucheza nyusika chache-chache kwenye mafilamu makubwa-makubwa kama vile Pearl Harbor (2001) na Catch Me if You Can (2002). Tangu hapo, Garner ameonekana kwenye nyusika kadha wa kadha akiwa kama mwigizaji mwandamizi vilevile mwigizaji mkuu kwenye mamiradi makubwa ikiwa ni pamoja na Daredevil (2003), 13 Going on 30 (2004) na Juno (2007). Ameolewa na mwigizaji na mwongozaji wa filamu Ben Affleck, ambaye kwa pamoja wameweza kujipatia watoto wawili wa kike.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Garner ni wa pili kuzaliwa katika familia ya watoto watatu wa kike waliozaliwa huko mjini Houston, Texas. Mama yake, Patricia Ann, alikuwa mwalimu wa lugha ya Kiingereza kutoka mjini Oklahoma, na baba yake, Bill John Garner, alifanyakazi kama mhandisi wa kemikali katika Union Carbide. Wakati alivyokuwa na umri wa miaka minne, kazi ya baba yake na Union Carbide iliwahamisha kuelekea mjini Princeton, West Virginia, na kisha baadaye mjini Charleston, West Virginia, ambapo Garner aliweka makazi hadi alipofikisha kipindi chake cha miaka ya chuo.[2] Alimsifia dada yake mkubwa, Melissa Lynn Garner Wylie, ambaye anaishi mjini Boston, Massachusetts, kama chanzo cha mafanikio yake.[3] Mdogo wake wa kike ni Susannah Kay Garner Carpenter.[4]
Msimamo wa Garner kiukuaji ni pamoja na kwenda kanisani kila Jumapili, hapaki majipambo ya usoni wala vibikini, na kusubiri hadi angalau alivyofikisha miaka 16 aruhusiwe masikio yake kutobolewa, ambapo, baadaye alileta mzaha kidogo, kaifanya familia yake "kuwa mbali kidogo na Uamish."[5][6] Ameanza kuchukua masomo ya ballet akiwa na umri wa miaka mitatu hadi kipindi chake chote cha ujana, lakini hajajibidisha yeye mwenyewe ili kufikia kiwango cha ballerina wa kisasa.[7] Garner alisoma katika shule ya George Washington High School ya mjini Charleston, West Virginia. Mnamo mwaka wa 1990, alijiunga na Chuo Kikuu cha Denison kilichopo mjini Ohio, ambapo alijikita zaidi katika masuala ya uigizaji na kufanya kazi kadha wa kadha kuhusiana na masuala ya utayarishaji na tamthilia.[8] Baada ya kuhitimu chuoni Denison, ambapo alijiunga na umoja wa kina dada wa Pi Beta Phi, kunako mwaka wa 1994.[9]
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 19 Oktoba 2000, Garner ameolewa na mwigizaji Scott Foley, ambaye alikutana naye kwenye seti ya tamthili ya Felicity kunako 1998. Baada ya kutengana na Foley mnamo mwezi wa Machi 2003, Garner amefungua faili la talaka kunako mwezi wa Mei 2003, na kutaja tofauti zao ambazo haziwezi kupatanishwa, na wawili hao wakatalikiana rasmi kunako tar. 30 Machi 2004.[10] Kufuatia kutengana kwake, Garner akaanza kutembea na mwigizaji-mshirika mwenzake kwenye Alias Michael Vartan kuanzia mwezi wa Agosti 2003 hadi Machi 2004.[11][12]
Wakati fulani katikati mwa 2004, Garner ameanza kutembea na mwigizaji-mshirika wa katika Daredevil Ben Affleck na wawili hao walionesha uhusiano wao mbele ya kadamnasi wakiwa kama wapenzi waliohudhuria katika siku ya ufunguzi wa Boston Red Sox-World Series kunako Oktoba 2004.[13] Tangu uhusiano wake na Affleck, kwanza akiwa kama demu wake na kisha baadaye kuwa mkewe.[14]
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]Filamu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
1997 | In Harm's Way | Kelly | |
1997 | Deconstructing Harry | Mwanamke katika Eleveta | |
1997 | Washington Square | Marian Almond | |
1997 | Mr. Magoo | Stacey Sampanahodrita | |
1998 | 1999 | Annabell | Jina lingine: Girls & Boys |
2000 | Dude, Where's My Car? | Wanda | |
2001 | Pearl Harbor | Nurse Sandra | |
2001 | Rennie's Landing | Kiley Bradshaw | Alternative title: Stealing Time |
2002 | Catch Me If You Can | Cheryl Ann | Uhusika wa Kuuza Sura |
2003 | Daredevil | Elektra Natchios | |
2004 | 13 Going on 30 | Jenna Rink mkubwa | |
2005 | Elektra | Elektra Natchios | |
2006 | Catch and Release | Gray | |
2007 | The Kingdom | Janet Mayes | |
2007 | Juno | Vanessa Loring | Amechaguliwa—Online Film Critics Society Award for Best Supporting Actress Amechaguliwa—Broadcast Film Critics Association Award for Best Cast |
2009 | Ghosts of Girlfriends Past | Jenny Perotti | |
2009 | The Invention of Lying | Anna | |
2010 | Valentine's Day | Julia Fitzpatrick | |
2011 | Butter | Laura Pickler | Inatengenezwa |
2011 | Arthur | Susan Johnson |
Television
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Lua error in Module:Citation/CS1/Configuration at line 2059: attempt to index a boolean value.
- ↑ Allmovie, Jennifer Garner Archived 8 Septemba 2014 at the Wayback Machine.. The New York Times. Retrieved on 12 Desemba 2006.
- ↑ Pringle, Gill. "Jennifer Garner: Actress with the ex factor." Archived 12 Desemba 2010 at the Wayback Machine. The Independent. Retrieved on 12 Februari 2010.
- ↑ Lua error in Module:Citation/CS1/Configuration at line 2059: attempt to index a boolean value.
- ↑ Rader, D. She's Reaching For Happiness—Again Parade magazine, 11 Aprili 2004. Retrieved on 8 Aprili 2009.
- ↑ Lights..... Cameras...... Action Mum! News of the World Sunday magazine, pp67-70, 4 Novemba 2007.
- ↑ Murray, R, Interview with Jennifer Garner Archived 27 Septemba 2011 at the Wayback Machine.. About.com. 12 Aprili 2004. Retrieved on 12 Desemba 2006.
- ↑ Lua error in Module:Citation/CS1/Configuration at line 2059: attempt to index a boolean value.
- ↑ Lua error in Module:Citation/CS1/Configuration at line 2059: attempt to index a boolean value.
- ↑ Bonin, L. "Felicitous Split Archived 15 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.". Entertainment Weekly. 15 Oktoba 2003. Retrieved on 13 Desemba 2006.
- ↑ Susman, G, "Undercover Work Archived 14 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.". Entertainment Weekly. 14 Agosti 2003. Retrieved on 13 Desemba 2006.
- ↑ Buzzle Staff and Agencies, "Garner & Vartan Split?". Buzzle.com. 24 Machi 2004. Retrieved on 23 Januari 2007.
- ↑ "Ben: I'm so batty about Jen", Mirror, 2004-10-27. Retrieved on 2010-02-11.
- ↑ Koltnow, Barry. "Elektra-fying", The Courier-Mail, 2005-01-13. Retrieved on 2010-02-11.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Jennifer Garner at the Internet Movie Database
- Jennifer Garner at the Internet Broadway Database
- Jennifer Garner katika Movies.com
- Jennifer Garner katika People.com
- Jennifer Garner katika Yahoo! Movies