California Love
“California Love” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya 2Pac featuring Dr. Dre and Roger Troutman kutoka katika albamu ya All Eyez On Me | |||||
Imetolewa | Desemba 1995 | ||||
Muundo | 12-inch single, CD single | ||||
Imerekodiwa | Oktoba 1995 | ||||
Aina | Hip hop | ||||
Urefu | 4:45 Single version 6:25 Album version (Remix) | ||||
Studio | Death Row | ||||
Mtunzi | Joe Cocker, Woodrow Cunningham, Norman Durham, Mikel Hooks, Ronald Hudson, Christopher Stainton, Larry Troutman, Roger Troutman, James Anderson, Tupac Shakur, | ||||
Mtayarishaji | Dr.Dre | ||||
Certification | 2x Platinum (RIAA) Gold (CRIA)[1] | ||||
Mwenendo wa single za 2Pac featuring Dr. Dre and Roger Troutman | |||||
| |||||
Mwenendo wa singles za single Dr. Dre | |||||
|
"California Love" ni wimbo wa hip hop ulioimbwa na 2Pac akishirikiana na Dr. Dre na Roger Troutman. Wimbo ulitolewa ukiwa kama single ya kurudi kwa 2Pac juu ya kutoka kwake jela mnamo 1995. Toleo mashuhuri la remix la wimbo huu limeonekana kwenye albamu-mbili za pamoja ya All Eyez on Me mnamo 1996. Wimbo huu huenda ukawa moja kati ya nyimbo maarufu za 2Pac yenye mafanikio zaidi, kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100 kwa majuma mawili (kama Double-A side single pamoja na "How Do U Want It"). Wimbo ulipata kuchaguliwa kwenye Grammy Award kama Rap Bora ya Msanii wa Kujitegemea na Rap Bora Ilioimbwa na Wasanii Wawili (pamoja na Dr. Dre na Roger Troutman) mnamo 1997.
Toleo halisi la wimbo huu halikupatikana kwenye albamu yoyote ya studio ya Shakur, lakini inaweza kupatikana kwenye kompilesheni ya Vibao Vikali vya Shakur.
Mlio wa wimbo umechukuliwa kutoka katika wimbo wa Joe Cocker wa "Woman to Woman", na uorodheshaji mistari ya "California knows how to party" -lifanywa katika Wilaya ya Los Angeles na kiitikio kuimbwa na Roger Troutman. Sauti za "In the City of Compton" na miji mingine na "California knows how to party" imechukuliwa kutoka kwa Ronnie Hudson na Street People's "West Coast Poplock". Remix yake imeingiziwa na sampuli ya wimbo wa "Intimate Connection" wa Kleeer uliotungwa na Norman Durham na Woody Cunningham.
"California Love" ulikuwa wimbo pekee wa Shakur kuingizwa kwenye orodha ya Rolling Stone ya mwaka wa 2004, Nyimbo Kali 500 za Muda Wote, na kupewa nafasi ya #346 na #51 kwenye VH1, Nyimbo Kali 100 za Miaka ya 1990.
Historia na utunzi
[hariri | hariri chanzo]California Love ulikuwa wimbo mmoja au wa pili kutayarishwa na Dre kwenye All Eyez on Me "California Love" na "Can't C Me", sehemu ya mwanzo wa wimbo kuna mistari mitatu iliomshirikisha Dr. Dre akirap. Nakala pekee ya kipengele hiki kwa sasa kinamilikiwa na DJ Jam, DJ binafsi wa Snoop Dogg. Sehemu ya kwanza ya Dre ilikuwa haija haririwa na ilirekodiwa nyumbani tu, na kwa maana hiyo, utofauti wa matoleo yalikuja kuingizwa hapo baadaye kwenye 2Pac Greatest Hits vilevile How Do U Want It (CD Maxi Single).
2Pac alisikia sehemu ya kwanza ya Dre wakati yupo katika studio ya Dre ya nyumbani na akamtaka Dre aingize maujanja yake kwenye wimbo huu. Dre alifanya mamixi kadhaa kwenye All Eyez On Me ikiwa kama matakwa ya Dre kutaka kutumia toleo halisi la wimbo huu aingize kwenye albamu yake, kwa hiyo All Eyez On Me imechukua toleo la remix la wimbo wakati toleo halisi la wimbo limekwenda katika albamu ya Dre.
Video mbili zilipigwa wakati mmoja na kutolewa na kupigwa kwenye MTV mwishoni mwa mwezi Desemba 1995. Toleo halisi lilitayarishwa na Hype Williams likiwa na Mandhari ya Mad Max (Sehemu ya 1 ya video), toleo la pili linaanza na 2Pac ana amka kutoka ndotoni, ambapo toleo halisi la Mad Max na mjengo wa sherehe unamkaribisha Pac katika Death Row.
Kimuziki, wimbo umechukua sampuli ya piano ya albamu ya kwanza ya Joe Cocker, Critical Beatdown.
Wimboni Roger anaimba "shake it, shake it baby", anarejea kipengele cha wimbo aliotumia kwenye single yake ya mwaka wa 1982 ,Zapp, "Dance Floor".
Muziki wa video
[hariri | hariri chanzo]Yapo matoleo mawili ya muziki wa video. Video ya kwanza (iliongozwa na Hype Williams) ilitengenezwa kutokana na filamu ya Mad Max Beyond Thunderdome, na kuchukua nafasi kwenye jangwa mnamo mwaka wa 2095. Washiriki waliokuwemo ni pamoja na mwimbaji George Clinton akiwa kama mwasi mkuu wa kikabila, mwigizaji Chris Tucker[2] (kipindi hicho alikuwa akijulikana kwa uhusika wake pekee wa kwenye filamu ya Friday) anacheza kama mwasi mkuu wa kikabila yes-man, Tony Cox kama mjeshi kijeba na Roger Troutman (zamani alikuwa na bendi ya Zapp) amebeba kisanduku cha kuongea. Upigaji picha umechukua nafasi mahali pa ajabu na vumbi la haja, ilijulikana sana kutoka katika filamu yenyewe. Inaishia na maneno ya To Be Continued. Toleo lingine, umejuimusha mikato ya remix ya wimbo, umeondoshwa chukulio la mwisho na kumwonesha 2Pac na Dre wanataja miji ya West Coast.
Toleo la pili limetokana na toleo la remix ya wimbo kutoka katika albamu ya All Eyez On Me, na mwendelezo wa hadithi ya video ya awali. Msingi wa video ya awali ilikuwa ni ndoto 2Pac ambayo alikuwa akiiota. Na alipoamka, akajikuta kitandani kwake pembeni akiwa na mwanamke. Dr. Dre akampigia simu na kumwambia kwamba aende nyumbani kwake wakajirushe na sherehe. Sehemu zote zilizobakia za video zilipigwa nyumbani tu na kushirikisha watu kadhaa walionekana ndani yake, almaarufu Roger Troutman ambaye kwa sasa anaonekana akipiga piano, na ugeni ualikwa kutoka kwa DJ Quik, Big Syke, Danny Boy, Jodeci, Deion Sanders, B-Legit, na E-40. Video ilitengenezwa kwa ajili ya remix ya wimbo.
Video ya kwanza ilichaguliwa kwenye MTV Video Music Award kwa ajili ya Best Rap Video mnamo 1996. Imefikia #9 kwenye 10 bora za MTV 100 Greatest Videos Ever Made kwenye orodha ya 1999. Mnamo mwezi wa Aprili 2005 imepata doa la nishani ya shaba kwenye MTV2 na XXL 25 Greatest West Coast Videos. Pia imefaulu #1 kwenye French MTV 100 Greatest Rap Music Videos mnamo 2006.
Wahusika
[hariri | hariri chanzo]- Mtunzi - Tupac Shakur
- Vinanda - Sean 'Barney' Thomas
- Ngoma - Carl 'Butch' Small
- Mtayarishaji, Mixing, Rap Shirikishi (Rap) - Dr. Dre
- Sauti, Talkbox - Roger Troutman
- Sauti za nyuma: Danette Williams, Dorothy Coleman, Barbara Wilson
- Mhandisi : Keston E. Wright
- Msaidi wa Matayarisho: Larry Chatman
- Uongozaji wa Video: Hype Williams
Tanbihi na marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-11-22. Iliwekwa mnamo 2010-05-11.
- ↑ Wilson, Elliott. "XXL", Pop Shots, Harris Publications, Aprili 2005, pp. 131–135.