[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Cagliari Calcio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Cagliari Calcio (maarufu kama Cagliari; matamshi ya Kiitalia: [ˈkaʎʎari]) ni klabu ya mpira wa miguu huko Italia. Klabu hii kwa sasa inacheza katika Serie A.

Uchezaji bora wa klabu hiyo Ulaya ulionekana kwenye mashindano ya kuwania Kombe la UEFA la mwaka 1993-94, ilitolewa na klabu ya Inter milan katika hatua ya nusu fainali.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya Serie A

[hariri | hariri chanzo]
Klabu ya Cagliari (mwaka 1930-1931)

Cagliari walikuwa mabingwa wa kwanza wa Serie C wakati wa msimu wa mwaka 1951-52; kabla ya hapo kwenye ligi, ubingwa ulishirikisha timu zaidi ya moja.

Mnamo miaka ya 1950 Cagliari ilipandishwa Serie B.

Mnamo mwaka 1954 walishushwa na kupelekwa Serie C kwa sababu ya kushuka kiwango cha uchezaji. Baada ya kushuka kwenye Serie C mwanzoni mwa mwaka 1960, Cagliari iliongeza kasi na ubora wa uchezaji na hatimaye ikafanikiwa kupandishwa kwenye Serie A mnamo mwaka 1964.

Klabu ya Cagliari ilicheza katika uwanja wa Stadio Sant'Elia mwaka 1970-2017

Klabu ya Cagliari ilihama kutoka katika uwanja wa Stadio Amsicora kwenda katika uwanja wa Stadio Sant'Elia mnamo mwaka 1970, baada ya kushinda taji lao pekee la ligi.

Mizozano na baraza la mji juu ya ukarabati wa uwanja ilimaanisha kuwa Cagliari alicheza michezo yao ya mwisho ya nyumbani ya mwaka 2011-12 huko Stadio Nereo Rocco katika Peninsula ya Italia.

Kwa misimu mingi uliofuata, klabu ya Cagliari ilicheza kwenye uwanja wa Stadio Is Arenas karibu na manispaa ya Quartu Sant'Elena.Uwanja wa Sant'Elia ulibomolewa mnamo mwaka 2017, na kilabu ilihamia uwanja wa Sardegna Arena.

Mataji ya kitaifa

[hariri | hariri chanzo]
  • Serie A:
    • Washindi (1): 1969–1970
  • Serie B:
    • Washindi (1): 2015–2016
  • Serie C / Serie C1:
    • Washindi (4): 1930–1931, 1951–1952, 1961–1962, 1988–1989
  • Coppa Italia Serie C:
    • Washindi (1): 1988–1989
  • Campionato Sardo di I Divisione:
    • Washindi (1): 1936–37

Mataji ya Ulaya

[hariri | hariri chanzo]

UEFA Cup:

  • Hatua ya nusu fainali (1): 1993–1994

Wachezaji

[hariri | hariri chanzo]

Kikosi cha sasa( mwaka 2020)

[hariri | hariri chanzo]

Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.

Na. Nafasi Mchezaji
1 Brazil GK Rafael
3 Italia DF Federico Mattiello (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Atalanta B.C.)
4 Ubelgiji MF Radja Nainggolan (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Inter Milan)
8 Italia MF Luca Cigarini
10 Brazil MF João Pedro
12 Italia DF Fabrizio Cacciatore
15 Estonia DF Ragnar Klavan
17 Uruguay MF Christian Oliva
18 Uruguay MF Nahitan Nández
19 Italia DF Fabio Pisacane
20 Uruguay MF Gastón Pereiro
Na. Nafasi Mchezaji
21 Moldova MF Artur Ioniță
23 Italia DF Luca Ceppitelli (Kapteni)
24 Italia MF Paolo Faragò
26 Italia FW Daniele Ragatzu
28 Italia GK Alessio Cragno
30 Italia FW Leonardo Pavoletti
33 Italia DF Luca Pellegrini (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Juventus)
34 Italia GK Giuseppe Ciocci
40 Poland DF Sebastian Walukiewicz
43 Italia FW Alberto Paloschi (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya SPAL)
90 Uswidi GK Robin Olsen (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya A.S. Roma)
99 Argentina FW Giovanni Simeone (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Fiorentina)

Barani Ulaya

[hariri | hariri chanzo]

Kombe la mabingwa wa Ulaya

[hariri | hariri chanzo]
Msimu Mzunguko Klabu Nyumbani Ugenini Jumla
1970–1971 Mzunguko wa kwanza Ufaransa Saint-Étienne 3–0 0–1 3–1
Mzunguko wa pili Hispania Atlético Madrid 2–1 0–3 2–4

Kombe la UEFA

[hariri | hariri chanzo]
Msimu Mzunguko Klabu Nyumbani Ugenini Jumla
1972–1973 Mzunguko wa kwanza Ugiriki Olympiacos 0–1 1–2 1–3
1993–1994 Mzunguko wa kwanza Romania Dinamo București 2–0 2–3 4–3
Mzunguko wa pili Uturuki Trabzonspor 0–0 1–1 1–1
Mzunguko wa tatu Ubelgiji Mechelen 2–0 3–1 5–1
Robo fainali Italia Juventus 1–0 2–1 3–1
Nusu fainali Italia Inter Milan 3–2 0–3 3–5


Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungu vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: