[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Awkwafina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Awkwafina
Amezaliwa2 June 1988
UtaifaMmarekani
Majina mengineAwkwafina
MhitimuChuo Kikuu cha Albany, SUNY (Shahada ya Sanaa)
Kazi yakeMwigizaji, Mwimbaji, Mtayarishaji wa Filamu
Miaka ya kazi2005-hadi sasa

Nora Lum[1] (anajulikana kitaaluma kama Awkwafina; amezaliwa Stony Brook, New York,[2] Juni 2, 1988)[3] ni mwigizaji, mwimbaji na mchekeshaji wa Marekani.

Alipata umaarufu mnamo mwaka 2012 wakati wimbo wake uliyoitwa "My Vag" uliposambaa katika YouTube. Kisha alifuatia kutoa albamu yake ya kwanza iliyoitwa Yellow Ranger (2014), na akawa akiigiza kwenye tamthilia zenye maudhui ya vichekesho iliyoitwa MTV Girl Code (2014-2015). Aliendelea na kuanza kuigiza katika filamu za vichekesho kama vile Neighbors 2: Sorority Rising (2016), Ocean's 8 (2018), Crazy Rich Asians (2018) na Jumanji: The Next Level (2019). Na baada ya kuigiza kama binti mwenye huzuni katika filamu ya The Farewell (2019) kulimfanya aweze kushinda Tuzo ya Golden Globe. Tangu 2020, Awkwafina amekuwa mtengenezaji, mwandishi, na mtayarishaji mkuu wa mfululizo wa tamthilia ya Vichekesho iliyoitwa Awkwafina Is Nora From Queens. Mnamo mwaka 2021, aliigiza kama Katy katika filamu ya Marvel Cinematic Universe Shang-Chi and Legend of the Ten Rings[4]. Pia ameigiza sauti katika filamu za katuni kama vile Storks (2016), The Angry Birds Movie 2 (2019), Raya and the Last Dragon (2021), The Bad Guys (2022), The Little Mermaid(2023), Migration (2023), na Kung Fu Panda 4 (2024).

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Baba yake anaitwa Wally Lum, Mmarekani mwenye asili ya Kichina, na mama yake Tia Lum, Mmarekani mwenye asili ya Kikorea[5]. Baba yake alifanya kazi katika idara ya teknolojia ya habari, na familia yake ilikua inafanya biashara ya kuhudumia mikahawa, babu yake alihamia Marekani [6]katika miaka ya 1940, na akafungua mgahawa wa Kikantoni wa Lum's huko Flushing, Queens[7],ukiwa ni mojawapo ya migahawa ya kwanza ya Kichina kuanzishwa Queens. Mama yake alikuwa mchoraji, alihamia Marekani akiwa pamoja na familia yake kutoka Korea Kusini mwaka 1972. Mama yake alifariki kutokana na shinikizo la damu katika mapafu mwaka 1992 ,Kipindi hiko Awkwafina alikuwa na umri wa miaka minne tu. Awkwafina alilelewa na baba yake , babu na bibi. Alikuwa karibu sana na nyanya yake mzaa baba aliyeitwa Powah Lum[8][9][10].

Awkwafina alilelewa Forest Hills, Queens, na alihudhuria Shule ya Fiorello H. LaGuardia, ambako alicheza tarumbeta na kufunzwa katika muziki wa aina ya jazz[11][12]. Akiwa na umri wa miaka 15, alijiita jina la kisanii la Awkwafina, lililo maanisha "hakika mtu niliyekandamizwa" na kubadilisha maisha yake na kua ya "utulivu na wa kutosheka" katika miaka yake akiwa chuo[13][14][15].

Amewataja Charles Bukowski, Anaïs Nin, Joan Didion, Tom Waits, na Chet Baker kama watu waliomuhamasisha na kumpa ushawishi katika maisha yake[16]. Kuanzia mwaka 2006 hadi 2008, alijifunza Mandarin katika Chuo Kikuu cha Lugha na Utamaduni cha Beijing ili aweze kuwasiliana na nyanyake mzaa baba[17]. Alihitimu katika uandishi wa habari na masomo ya wanawake katika Chuo Kikuu cha Albany, Chuo Kikuu cha Jimbo la New York na kuhitimu mwaka wa 2011.

  1. https://twitter.com/awkwafina/status/1008972165591523329
  2. Scott Feinberg (2019-11-10). "'Awards Chatter' Podcast — Awkwafina ('The Farewell')". The Hollywood Reporter (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
  3. 网易 (2020-01-06). "金球奖首个亚裔影后!奥卡菲娜获喜剧电影最佳女主". www.163.com. Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
  4. "Awkwafina on her Shang-Chi role: 'They made her a little bit different'". Radio Times (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
  5. "Awkwafina Opens Up About How the Death of Her Mother at 4 Years Old Changed Her Life". Peoplemag (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
  6. Rachel Chang (2017-02-25). "5 Things to Know About 'Ocean's Eight' Star Awkwafina". Us Weekly (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
  7. https://web.archive.org/web/20190331071848/http://kore.am/september-cover-story-awkwafina-establishing-her-presence/
  8. "Awkwafina: 'I was always the crazy one, the funny one. I'd do anything for a laugh'", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2018-06-17, ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2024-05-08
  9. "Awkwafina Opens Up About How the Death of Her Mother at 4 Years Old Changed Her Life". Peoplemag (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
  10. "Awkwafina Opens Up About How the Death of Her Mother at 4 Years Old Changed Her Life". Peoplemag (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
  11. Trinh, Jean (2013-03-14), "Meet Awkwafina: an Asian Female Rapper on Vaginas, Tackling Racism & More", The Daily Beast (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2024-05-08
  12. "Awkwafina New York State Writers Institute". www.albany.edu. Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
  13. Donnie Kwak (2017-05-23). "Awkwafina Won't Let You Forget Her Name". The Ringer (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
  14. "Crazy Rich Asians Star Awkwafina On Her Makeup Essentials". Into The Gloss. 2017-04-11. Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
  15. Tonya Burks (2017-03-29). "Awkwafina Got Fired From Her Office Job After Writing a Song Called "My Vag"". Galore (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
  16. "Awkwafina", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-05-03, iliwekwa mnamo 2024-05-08
  17. "新京报 - 好新闻,无止境". www.bjnews.com.cn. Iliwekwa mnamo 2024-05-08.