Adamu
Adamu (kwa Kiebrania: אָדָם maana yake mtu, mtu wa udongo, chaudongo, au wa udongo mwekundu) ni jina analopewa mtu wa kwanza katika Biblia. Anatajwa na Kurani pia.
Kadiri ya kitabu cha Mwanzo, alizaliana na mke wake Eva watu wote waliopo duniani, ambao kwa sababu hiyo wanaitwa binadamu; kwa namna ya pekee waliweza kuzaa wenyewe Kaini, Abeli na Seti.
Kanisa Katoliki linamheshimu kama mtakatifu kila tarehe 24 Desemba[1].
Katika Biblia
[hariri | hariri chanzo]Uumbaji wa watu wa kwanza unasimuliwa na kitabu cha Mwanzo mara mbili: katika 1,26-28 na katika 2,7-22.
Masimulizi hayo yanayotofautiana katika vipengele mbalimbali hayadai yachukuliwe kama habari za historia zinazoandikwa siku hizi. Yanatokana na tafakuri ya kina juu ya hali ya binadamu kwa lengo la kuelewa asili yake.
Katika Kurani
[hariri | hariri chanzo]Humo Adamu anatajwa kwa namna inayofanana na ile ya Biblia. Anahesabiwa kuwa mtume wa kwanza.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Adamu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |