[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

The Notorious B.I.G.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 02:44, 4 Julai 2024 na InternetArchiveBot (majadiliano | michango) (Rescuing 1 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.9.5)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
The Notorious B.I.G.
Jina la kuzaliwa Christopher George Latore Wallace
Amezaliwa (1972-05-21)Mei 21, 1972
New York City, New York, United States
Amekufa 9 Machi 1997 (umri 24)
Los Angeles, California, United States
Aina ya muziki Hip hop[
Kazi yake Rapa, mtunzi wa nyimbo, mwimbaji, mtayarishaji wa rekodi
Miaka ya kazi 1992–1997
Studio Bad Boy
Ame/Wameshirikiana na Sean Combs, Method Man, Junior M.A.F.I.A., Total, 112, The Commission
Tovuti www.badboyonline.com/notoriousbig

Christopher George Latore Wallace (anajulikana kama Biggie Smalls, jina la jambazi la kwenye filamu ya mwaka wa 1975 ya Let's Do It Again, "The Black Frank White", jina la mwuza madawa ya kulevya katika filamu ya mwaka wa 1990 King of New York),[1] na hasa kwa jina la kisanii The Notorious B.I.G.; 21 Mei 19729 Machi 1997) alikuwa rapa kutoka nchini Marekani.

Alikulia Brooklyn, mji wa New York City, Wallace amekua kwenye kipindi cha matatizo ya uigaji tabia chafu kwenye miaka ya 1980, hivyo basi akaanza kujishughulisha na uuzaji haramu wa dawa za kulevya akiwa bado bwana mdogo kabisa. Wakati Wallace ametoa albamu yake ya kwanza yenye jina la rekodi ya mwaka 1994 Ready to Die, alikuwa umbo la kati kwenye uwanja wa East Coast hip hop na kuongeza mwonekano wa New York kwa kipindi hicho wakati wasanii wa West Coast tayari wamekuwa maarufu kwenye nyanja kuu za hip hop kitambo. Mwaka uliofuatia, Wallace akaongoza marafiki zake wa utotoni hadi kwenye mafanikio ya kichati kupitia kundi la wafuasi wake la Junior M.A.F.I.A.. Wakati anarekodi albamu yake ya pili, Wallace alijishughulisha sana na masuala ya kigomvi ya East Coast-West Coast, ilitawala katika uwanja wa hip hop kwa kipindi hicho.

Mnamo tar. 9 Machi 1997, Wallace aliuawa na watu wasiojulikana wakati anaendesha gari huko mjini Los Angeles. Seti yake ya diski mbili ya Life After Death, ilitolewa baada ya siku kumi na tatu baadaye, imegonga nafasi ya kwanza #1 kwenye chati za albamu nchini Marekani na kutunukiwa Almasi mnamo mwaka wa 2000.[2] Wallace alitambulika sana kwa staili yake ya "kujiachia, anachana taratibu", uwezo wa kimashairi yanayoeleza tawasifu kimtindo. Tangu kifo chake, albamu mbili zaidi zilitolewa. MTV wamweka nafasi ya #3 kwenye orodha yao ya Ma-MC Wakali wa Muda Wote.[3]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Alizazaliwa kwenye Hospitali ya Mt. Mary, ingawa inadaiwa kwamba alikulia mjini Bedford-Stuyvesant sehemu ya Brooklyn, nyumba ambayo Wallace alikulia ipo karibu na Clinton Hill.[4] Wallace alikuwa mtoto pekee wa Voletta Wallace, mwalimu wa shule ya vidudu mwenye asili ya Jamaika, na George Latore, fundi wa kuchomelea na mwanasiasa wa muda mfupi wa Kijamaika. Baba'ke ameiacha familia wakati Wallace akiwa na umri wa miaka miwili, amemwacha mama'ke akifanya kazi mbilimbili ili aweze kumkuza mwanawe. akiwa katika shule ya Queen of All Saints Middle School, Wallace amefukuzwa darasani, ameshinda matuzo kadha wa kadha akiwa kama mwanafunzi bora wa somo la Kiingereza. He was nicknamed "Big" because of his size before he turned 10-years-old.[5] Akiwa na umri wa miaka 12, akaanza kuuza dawa za kulevya. Mama'ke, marakwamara anakuwa yu kazini, hakutambua suala la uuzaji wa dawa za kulevya hadi Wallace alipokuwa mtu mzima.[6]

Wallace akahamishia katika shule ya kulipia ya Romani Katoliki ambayo alihitimia hapo, kwa hiari yake, ameomba kujiunga na shule ya George Westinghouse Information Technology High School. Jay-Z na Busta Rhymes nao walikuwa wanafunzi wa shule hiyo pia. Kwa mujibu wa mama'ke, Wallace bado aliendelea kuwa mwanafunzi mzuri tu, lakini aliendeleza tabia zake za "ujanja wa matako" hadi katika shule mpya.[7] Akiwa na umri wa miaka 17, Wallace akaachilia mbali shule na kujihusisha zaidi na masuala ya kihalifu. Mwaka wa 1989, alitiwa mbaroni kwa kosa la umiliki wa silaha kinyume cha sheria huko mjini Brooklyn na kuhukumiwa kifungo cha nje kwa muda miaka mitano. Mwaka wa 1990, alitiwa tena nguvuni kwa kosa la kufanya fujo kwa kifungo chake cha nje. Mwaka mmoja baadaye, Wallace alitiwa tena nguvuni kwa kosa la kugushi dawa za kulevya huko mjini North Carolina. Ametumia takriban miezi tisa jela hadi hapo alipopata dhamana.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Studio albamu

[hariri | hariri chanzo]

Albamu zilitolewa baada ya kifo chake

[hariri | hariri chanzo]

Albamu za ushirikiano

[hariri | hariri chanzo]

Albamu za kompilesheni

[hariri | hariri chanzo]

  1. Reid, Shaheem; Bland, Bridget. Kash, Tim Notorious B.I.G.: In His Own Words, And Those of His Friends Archived 11 Machi 2007 at the Wayback Machine. MTV News, 2007-03-07. Retrieved on 2007-03-11
  2. "Top 100 Albums". RIAA. 4 Mei 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-01-22. Iliwekwa mnamo 2006-12-07.
  3. The Greatest MCs of All Time Archived 18 Machi 2015 at the Wayback Machine. MTV. Retrieved on 2006-12-26
  4. Franklin, Marcus. Much change in Biggie Smalls' neighborhood. Associated Press via Yahoo. 17 Januari 2009.
  5. Sullivan, Randall. "The Unsolved Mystery of the Notorious B.I.G.", Rolling Stone, 5 Desemba 2005. Retrieved on 2006-10-07. Archived from the original on 2009-04-29. 
  6. Touré "Biggie Smalls; Rap's Man of the Moment" The New York Times, 1994-12-18. Retrieved on 2008-03-26
  7. Coker, Cheo H. (8 Machi 2005). "Excerpt: Unbelievable - The Life, Death, and Afterlife of The Notorious B.I.G." Vibe. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-16. Iliwekwa mnamo 2006-10-07.

Soma zaidi

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons