[go: up one dir, main page]

Waziri Mkuu ni cheo cha kiongozi wa serikali. Neno lasema ya kwamba yeye ni mkubwa kati ya mawaziri wa serikali. Madaraka yake hutegemea na katiba ya nchi. Kwa kawaida cheo hiki kipo katika nchi ambako mkuu wa dola ambaye mara nyingi huitwa rais au pia mfalme (malkia) hashughuliki mwenyewe mambo ya serikali.

Kasimu Majaliwa,waziri mkuu wa Tanzania

Lugha inaweza kuwa tofauti kati ya nchi na nchi. Anaweza kuitwa pia "Rais wa Mawaziri", "Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mawaziri" au "Chansella".

Kuna hasa aina mbili za mawaziri wakuu kufuatana na katiba za nchi mbalimbali:

Waziri Mkuu katika muundo wa serikali ya kibunge

hariri
  • waziri mkuu kama kiongozi wa siasa ya nchi anachaguliwa na bunge.
    Mifano: Ethiopia, Uhindi, Uingereza au Ujerumani.
    Katika muundo huu nafasi ya rais au ya mfalme ni cheo cha heshima kama ishara ya umoja wa taifa. Waziri mkuu hutegemea kabisa idadi ya wabunge wanaoshikamana naye. Mkuu wa dola anaongezeka umuhimu kama bunge limegawanywa na hakuna uwingi ulio wazi kwa mgombea mmoja wa nafasi ya waziri mkuu.
    • Katiba zinatofautiana kama mawaziri wote wako tu kwa mapenzi ya waziri mkuu au kama bunge linawachagua mmoja-mmoja. Hii inamaanisha tofauti kama waziri ana msimamo mbele ya waziri mkuu au kama hana.

Waziri Mkuu katika muundo wa serikali ya kiraisi au kifalme

hariri
  • waziri mkuu kama kiongozi wa serikali tu chini ya usimamizi wa rais au mfalme anayeshika madaraka makubwa.
    Mifano: Tanzania, Ufaransa.
    Katika muundo huu rais huchaguliwa na wananchi wote. Yeye anamteua waziri mkuu, mara nyingi hata mawaziri wenyewe.

Katiba inaweza kusema ya kwamba rais ni huru kumchagua waziri mkuu hata bila kujali idadi ya wabunge wake bungeni. Katika mfumo huu waziri mkuu ni zaidi kama meneja wa kazi ya serikali.

Lakini kuna mifano ambako katiba inampa rais na pia waziri mkuu kila mmoja madaraka yake. Kwa mfano rais kusimamia mambo ya jeshi na usalama pamoja na siasa ya nje na waziri mkuu kusimamia siasa ya ndani na ya kiuchumi. Hapo waziri mkuu atakuwa na uhuru zaidi mbele mkubwa wake.

Mifano ya nchi wenye mawaziri wakuu

hariri