[go: up one dir, main page]


Sulfuri (pia salfa au kibiriti, ing. sulfur) ni elementi simetali yenye namba atomia 16 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 32.065. Alama yake ni S. Kwenye hali sanifu ni imara kuwa fuwele zenye rangi ya njano.

Sulfuri (salfa, kibiriti)
Sulfuri ikiwaka yayeyuka kuwa kiowevu chekundu; rangi ya moto ni buluu.
Sulfuri ikiwaka yayeyuka kuwa kiowevu chekundu; rangi ya moto ni buluu.
Jina la Elementi Sulfuri (salfa, kibiriti)
Alama S
Namba atomia 16
Mfululizo safu Simetali
Uzani atomia 32.065
Ugumu (Mohs) 2.0
Kiwango cha kuyeyuka 388.36 K (115.21 °C)
Kiwango cha kuchemka 717.8 K (444.6 °C)
Asilimia za ganda la dunia 0.05 %
Hali maada imara

Kutokea duniani

hariri

Hutokea duniani kama elementi tupu hasa kwenye volkeno, lakini zaidi kwenye kampaundi ndani ya madini ya sulfidi. Leo hii inapatikana kutokana na mafuta ya petroli wakati yakisafishwa.

Sulfuri ni elementi ya lazima kwa maada hai na seli zote zinatumia sulfuri.

Matumizi ya kibiashara

hariri

Matumizi yake ya kiuchumi ni hasa kwa mbolea ya chumvi, lakini pia katika baruti, viberiti na dawa za kuulia wadudu.

Sulfuri - kibiriti

hariri

Jina jingine la sulfuri ni "kibiriti" (kutoka Kiarabu كبريت) linalopatikana kwa mfano katika tafsiri za Biblia (k.m. Luka 17,29, Ufunuo 9,17). Matumizi ya neno hilo kwa ajili ya "vibiriti" yalijitokeza kwa sababu mwanzoni kichwa cha vijiti kilikuwa na mchanganyiko wa dawa zenye sulfuri au "kibiriti" ndani yake. Hivyo tafsiri nyingine ya "vibiriti" ni "vijiti vyenye sulfuri".

Viungo vya Nje

hariri

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sulfuri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.