Wadudu
Wadudu | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Maumbile ya mdudu: A. Kichwa, B. Toraksi (kidari), C. Fumbatio, 1. Kipapasio, 2. Mandibuli (taya), 3. Laboro (mdomo wa juu), 4. Palpi ya maxila, 5. Klipei, 6. Paji, 7. Verteksi (pia ya kichwa), 8. Pronoto, 9. Skutelo, 10. Elitra (mabawa ya mbele), 11. Pingili, 12. Spirakulo, 13. Mguu wa mbele, 14. Mguu wa kati, 15. Mguu wa nyuma.
| ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Nusungeli na oda:
|
Wadudu wa kweli (tazama mdudu) ni kundi la arithropodi wadogo kiasi ambalo lina spishi nyingi duniani. Kibiolojia wako katika ngeli ya Insecta.
Wadudu wanashirikiana kuwa na muundo wa mwili chenye pande tatu za kichwa mbele, kidari katikati na fumbatio nyuma, halafu jozi tatu za miguu na kwa kawaida jozi mbili za mabawa. Kwa nje kiwiliwili kinafunikwa kwa khitini yenye kazi ya kiunzi nje.
Hadi sasa wataalamu waliainisha zaidi ya spishi milioni 1 za wadudu na makadirio ni kwamba kuna spishi nyingi zaidi, labda hadi milioni 30.
Wadudu wanaishi takriban kila mahali duniani. Spishi nyingi zinapatikana katika sehemu za tropiki na idadi inapungua kwenye baridi. Lakini kuna hata spishi moja iliyopatikana Antaktika. Wadudu ni wachache sana baharini lakini hata humo kuna spishi chache.
Uainishaji
haririUainishaji wa wadudu umebadilika sana tangu utumiaji wa uchanganuzi wa ADN umeanza. Mfano wa mwainisho wa hivi karibuni unafuata:
- Ngeli Insecta
- Nusungeli Monocondylia
- Oda Archaeognatha
- Kladi (kundi bila tabaka) Dicondylia
- Nusungeli Apterygota
- Oda †Monura
- Oda Thysanura (Wadudu mikia-mitatu)
- Nusungeli Pterygota
- Ngeli ya chini Palaeoptera
- Oda †Palaeodictyoptera
- Oda †Megasecoptera
- Oda †Archodonata
- Oda †Diaphanopterodea
- Oda †Meganisoptera
- Oda Ephemeroptera (Wadudu siku-moja)
- Oda Odonata (Kereng'ende)
- Ngeli ya chini Neoptera
- Oda ya juu Exopterygota
- Oda †Titanoptera
- Oda †Protorthoptera
- Oda Plecoptera (Wadudu mabawa-msuko)
- Oda Embioptera (Wasokotaji-hariri)
- Oda Zoraptera (Wadudu-malaika)
- Oda Dermaptera (Wadudu-koleo)
- Oda Orthoptera (Wadudu mabawa-manyofu: panzi, nzige, nyenje, chenene, senene n.k.)
- Oda Phasmatodea (Wadudu-kijiti)
- Oda Notoptera (Wadudu-barafu, watambaaji-miamba)
- Oda ya juu Dictyoptera (imependekezwa)
- Oda Blattodea (Mende na mchwa)
- Oda Mantodea (Vivunjajungu)
- Oda ya juu Paraneoptera (imependekezwa)
- Oda Psocoptera (Nzi-gome, chawa-vitabu)
- Oda Thysanoptera (Tiripsi)
- Oda Phthiraptera (Chawa)
- Oda Hemiptera (Wadudu mabawa-nusu: kunguni, vidukari, nzi weupe, wadudu-gamba, vidung'ata)
- Oda ya juu Endopterygota
- Oda Hymenoptera (Wadudu mabawa-viwambo: nyuki, nyigu, sisimizi n.k.)
- Oda Coleoptera (Mende-kibyongo, bungo, fukusi, visaga)
- Oda Strepsiptera (Wadudu mabawa-potwa)
- Oda Raphidioptera (Wadudu shingo-ngamia)
- Oda Megaloptera (Wadudu mabawa-makubwa)
- Oda Neuroptera (Wadudu mabawa-vena)
- Oda ya juu Mecopteroidea (imependekezwa)
- Oda Mecoptera (Wadudu mabawa-marefu: wadudu-nge n.k.)
- Oda Siphonaptera (Viroboto)
- Oda †Protodiptera (Nzi wa kale)
- Oda Diptera (Wadudu mabawa-mawili: nzi, mbu n.k.)
- Oda ya juu Amphiesmenoptera (imependekezwa)
- Oda Trichoptera (Wadudu mabawa-manyoya)
- Oda Lepidoptera (Wadudu mabawa-vigamba: vipepeo, nondo)
- Oda ya juu Exopterygota
- Ngeli ya chini Palaeoptera
- Nusungeli Apterygota
- Nusungeli Monocondylia
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wadudu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |