Nazareti
mji katika Israeli; inayokaliwa zaidi na raia Waislamu-Waarabu wa Israeli; kitovu cha hija ya Kikristo kama nyumba ya utoto ya Yesu
Nazareti (الناصرة kwa Kiarabu, נצרת kwa Kiebrania) ni mji wenye watu 77,445[1] upande wa kaskazini wa nchi ya Israeli, ambao kihistoria unajulikana kama Galilaya.
Wakazi wengi ni raia wa Israeli wanaoongea Kiarabu na kufuata dini za Uislamu (68,7%) na Ukristo (31,3%).
Nazareti unajulikana kama mji walipokulia Bikira Maria na mwanae Yesu Kristo, ambaye kadiri ya Injili, ingawa alizaliwa Bethlehemu, alikuwa anatajwa kama Mnazareti.
Marejeo
hariri- ↑ "Population in the Localities 2019" (XLS). Israel Central Bureau of Statistics. Retrieved 16 August 2020.
Viungo vya nje
hariri- The New Official site of Nazareth City Archived 12 Desemba 2019 at the Wayback Machine.
- Nazareth City Website Archived 13 Aprili 2009 at the Wayback Machine.
- Nazareth in the Jewish Encyclopedia
- W.R.F. Browning, Oxford Dictionary of the Bible: Nazareth
Makala kuhusu Israeli bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |