Kiatu
Kiatu ni bidhaa yenye lengo la kulinda na kustarehesha mguu wa binadamu wakati wa kufanya shughuli mbalimbali. Pia kutumika kama bidhaa ya mapambo na mitindo, hasa kutokana na aina mbalimbali sana, tena tofauti kati ya utamaduni mmoja na utamaduni mwingine.
Zaidi ya hayo, mitindo mara nyingi imefanya wengi kubuni mambo, kama vile viatu vya visigino virefu au tambarare. Tofauti ya gharama yake inatumika pia kujenga matabaka kati ya watu. Viatu viliiyotolewa na wabunifu maarufu vinaweza kuwa vya vifaa ghali, na kuuzwa kwa mamia au hata maelfu ya dola za Marekani.
Baadhi ya viatu vinaundwa kwa madhumuni maalum, kama vile buti iliyoundwa mahsusi kwa ajili ya kupanda milima au kuteleza juu ya theluji.
Kwa kawaida, viatu vimefanywa kutoka ngozi, mbao au turubai, lakini pia vinazidi kufanywa kutoka mpira, plastiki n.k.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiatu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |