Wavuvi
Wavuvi (kutoka kitenzi "kuvua"; kwa Kiingereza "fishermen") ni watu wanaofanya kazi ya kuvua samaki na wanyama wengine kutoka kwenye maji ya baharini, mitoni, ziwani au bwawani na hujipatia kipato kupitia kazi hii.
Kutokana na takwimu za FAO Ulimwenguni kote kuna watu milioni 38 duniani wanaofanya kazi ya kuvua au kufuga samaki na hivyo husaidia kukuza uchumi wa nchi. Mara nyingi wavuvi hutumia chombo cha kusafiria majini kama boti au mtumbwi lakini wengine wanakaa ufukoni na kuvua kutoka nchi kavu.
Vyombo vya uvuvi ni aina za nyavu zinazoweza kushika samaki na kuwavuta nje ya maji, ndoano au pia aina za mikuki inayolenga samaki walio karibu na uso wa maji.
Watu wengi hupata protini kwa kula windo la samaki.
Wavuvi wanaweza kuwa wataalamu wa kazi hiyo au kuifanya kama burudani tu; wanaweza kuwa wanaume au wanawake vilevile.
Uvuvi umekuwepo kama njia ya kupata chakula tangu kipindi cha enzi za mawe ya kati.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wavuvi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |