[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lango la Kanisa la Kaburi na Ufufuo.
Banda la kaburi la Yesu Kristo ndani ya kanisa.

Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu liko mjini Yerusalemu mahali ambako, kufuatana na mapokeo ya Ukristo, Yesu alisulubiwa, akawekwa kaburini na kufufuka siku ya tatu.

Kanisa hili laitwa "Kanisa la ufufuo" na Wakristo wenyeji Waorthodoksi (kwa Kiarabu: كنيسة القيامة kanisat-al-qiyama) na "Kanisa la Kaburi" kwa lugha nyingi za Ulaya.

Kufuatana na mapokeo ya mahali mwamba wa Golgota uliposimama msalaba wa Yesu na kaburi alikozikwa vyote vilikuwa karibu sana hivyo mahali pote pawili hufunikwa na jengo lilelile.

Historia ya jengo

[hariri | hariri chanzo]
Ramani ya kanisa la Kaburi

Habari za kwanza zinapatikana kutoka kwa Eusebi wa Kaisarea (275339) aliyeandika ya kwamba mahali pa kaburi la Yesu lilifunikwa na hekalu la Apolo, mungu mmojawapo wa Kiroma. Hii huaminiwa ilitokea baada ya mwaka 135, mji wa Yerusalemu ulipotangazwa kuwa mji wa Kiroma, na Wayahudi walikatazwa wasiingie tena.

Kaisari Konstantino Mkuu aliagiza mahali pafunuliwe tena na kanisa, la kwanza kujengwa juu ya kaburi, lililotabarukiwa tarehe 14 Septemba 335[1]. Kanisa hilo lilibomolewa na Waajemi waliovamia Yerusalemu mwaka 614. Likatengenezwa chini ya Kaisari Heraklio mnamo 630 likaheshimiwa na Waarabu Waislamu walioteka mji mwaka 637.

Kanisa lilibomolewa kabisa mara ya pili mwaka 1009 chini ya khalifa Al-Hakim bin-Amr Allah wa Misri. Likajengwa upya wakati wa vita ya misalaba mwaka 1149 na watawala Wakristo. Baada ya hao kufukuzwa jengo lilikabidhiwa na Waislamu kwa watawa Wafransisko ambao ni Wakatoliki.

Ushirikiano wa madhehebu

[hariri | hariri chanzo]

Katika karne za baadaye ikafuata mivutano kati ya madhehebu mbalimbali, hasa Wakatoliki na Waorthodoksi.

Tangu karne ya 19 kuna namna ya ushirikiano kati ya Waorthodoksi Wagiriki, watawa Wafransisko na Waorthodoksi wa Mashariki wa Armenia. Waorthodoksi wa Mashariki Wasyria, Wamisri na Waethiopia hushirikiana pia.

Funguo hutunzwa na familia ya Kiislamu.

Adhimisho la kila mwaka

[hariri | hariri chanzo]

Kumbukizi ya kulitabaruku inafanyika kila mwaka tarehe 13 Septemba[2].


Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.