[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Hazinadata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hazinadata (kwa Kiingereza: database) ni mfumo wa kuhifadhi na kutunza idadi kubwa ya data, kwa kawaida data za kidijiti. Inatakiwa kuruhusu upatikanaji wa data au sehemu za data kwa ajili ya watumiaji na programu zinazotumia data hizo.

Matumizi yake huendeshwa na injini ya hazinadata yaani programu ya kompyuta kuwekulia, kusahihisha na kufusia data zake.

Mfano sahili wa hazinadata ni orodha ya anwani yenye majina, anwani za makazi, za posta, za kazi pamoja na namba za simu, anwani za baruapepe, labda pia data za binafsi, kama vile tarehe ya kuzaliwa, majina ya familia n.k. jinsi watu wengi wanavyoitunza kwenye simu janja. Injini ya hazinadata inaweza kupanga data hizo kwa namna mbalimbali, kwa mfano kufuatana na eneo la makazi, kufuatana na umri, kazi, mwajiri au kwa namna nyingine.

Data zinatunzwa leo hii kwa fomati ya kidijiti kwenye kompyuta. Zamani data zilihifadhiwa kwenye vitabu, orodha, faili ya kadi na kadhalika. Tathmini ya data hizo ilichukua muda mrefu. Hazinadata za kisasa zinazotunzwa kwenye kompyuta zinaruhusu kufanya tahmini ya data nyingi kwa muda mfupi.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.