[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kibodi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kibodi ya kawaida kwa mfumo wa Marekani.

Kibodi (pia: Kiibodi[1], Kicharazio[2], Baobonye au Bodidota/Bodi ya dota[3]; kwa Kiingereza: keyboard) ni kifaa muhimu kinachomwezesha mtu kuweka maandishi na namba kwa tarakishi (kompyuta). Inafanywa na vibonye vingi kwa ajili ya kila herufi na alama nyingine zinazotumiwa mara kwa mara.

Kibodi ni pia sehemu ya chombo cha muziki k.v. piano, iliyo na vibonye vyenye rangi vinavyobonyezwa ili kutoa sauti.

Kwa tarakilishi nyingi ni kifaa kikuu cha kuingizia habari mashineni.

Kuna mifumo mbalimbali za baobonye kulingana na lugha.

Muundo wa kawaida kwa lugha zinazotumia alfabeti ya Kilatini ni QWERTY (hizi ni herufi 6 za kwanza).

Muundo huu unaweza kuchosha mikono na vidole. Ulianzishwa zamani za mashine za kupiga chapa na mfumo wa herufi ulilenga kutovurugisha mikono ya taipu. Siku hizi ni kama hakuna taipu tena, lakini watu waliozoea muundo umebaki vile.

Majina ya vibonyezo (keys)

[hariri | hariri chanzo]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kibodi ni kifaa cha kuingiza data kwenye kompyuta au vifaa vingine vya elektroniki kwa kutumia herufi, namba, na alama nyingine. Historia ya kibodi inaanzia katika miaka ya mapema ya karne ya 19 wakati ilianza kutumika kwa mashine za kuchapa.

Mashine za kwanza za kuchapa zilikuwa zikitumia kibodi za mekaniki ambazo zilikuwa na herufi zilizopangwa kwa njia ya kawaida. Mfano maarufu wa kibodi za awali ni Sholes and Glidden Typewriter ambayo ilizinduliwa mwaka 1873.

Kibodi za kisasa zilianza kujitokeza katika miaka ya 1960 na 1970, wakati teknolojia ya umeme ilianza kuchukua nafasi ya mifumo ya mekaniki. Kibodi za kompyuta za kwanza zilikuwa na muundo wa kawaida wa QWERTY, ambao bado unaendelea kutumika hadi leo.

Kwa miaka mingi, kibodi kimekuwa kifaa muhimu sana katika kompyuta na vifaa vingine vya elektroniki. Limekuwa likiboreshwa na kubuniwa upya mara kwa mara ili kuboresha ufanisi na urahisi wa matumizi. Leo, kibodi za kompyuta zina vifungo maalum kwa ajili ya kazi mbalimbali kama vile kupiga simu, kurekebisha sauti, au kufikia huduma za mtandao.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. KKS Kamusi Kuu ya Kiswahili, toleo la nne, TUKI 2019
  2. Kamusi Kuu ya Kiswahili
  3. Kamusi ya Karne ya 21, EMAC, BAKITA na KIE. ISBN: 998-702-097-6