[go: up one dir, main page]

Westside Connection

Westside Connection ni kundi la muziki wa rap na hip hop kutoka mjini Los Angeles, California, Marekani. Kundi linaongozwa na msanii Ice Cube, WC na Mack 10. Kundi lilitoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Bow Down, na kuweza kushika nafasi ya pili katika chati za Billboard 200 bora za mwaka wa 1996.

Westside Connection
Kutoka kushoto kuelekea kulia ni: WC, Ice Cube, Mack 10.
Kutoka kushoto kuelekea kulia ni: WC, Ice Cube, Mack 10.
Maelezo ya awali
Pia anajulikana kama WSCG (West-Side Connect Gang)
Asili yake Los Angeles, California, Marekani
Aina ya muziki West Coast hip hop, Gangsta rap, Rap za kisiasa
Miaka ya kazi 1994-
Studio Priority
Capitol
Da Lench Mob
Tovuti westsideconnection.org
Wanachama wa sasa
Ice Cube
WC
Wanachama wa zamani
Mack 10

Kundi liliazishwa wakati wa kipindi cha mzozo wa wasanii wa hip hop wa East Coast na West Coast, uliozuka baada ya kifo cha marehemu 2Pac. Hawa nao waliwahi kuwa na ugomvi na Cypress Hill, Common, na Q-Tip.

Wasifu

hariri

Baada ya kusimama kufanya kazi kwa muda mrefu, kundi likatoa albamu yao ya pili iliyokwendwa kwa jina la Terrorist Threats na ilitoka mnamo mwaka wa 2003, ikiwa imeachiwa na kibado chao mashuhuri cha "Gangsta Nation" kilichomshirikisha rapa Nate Dogg.

Mnamo mwaka wa 2005 Mack 10 aliondoka katika kundi kwa kufuatia kugombana na rapa mwenziwe - WC..[1]

Mnamo mwaka 2008, kulikuwa na fununu zilizoenea kuwa The Game huenda akajiunga na kundi hilo. Uvumi huu unatokana na mistari yake Ice Cube na WC walioimba katika nyimbo ya "Get Used To It" ambamo Game alisema kuwa anaweza kujiunga na Lench Mob (akiwa na maana ya kujiunga na Westside Connection).

Wakati The Game alipoukana uwanachama huo, mda mfupi Ice Cube akiwa katika mahojiano alikiri kuwa mambo hayo yana ukweli ndani yake. Na pale alipoulizwa kuhusu The Game kujiunga na kundi, alijiinamia chini na kusema "labda". [2]

Ugomvi wao na Cypress Hill

hariri

Muziki

hariri

Albamu zao

hariri
Mwaka Jina Chati iliyoshika[3][4] Mara mwisho katika RIAA certification[5][6][7]
Billboard Hot 200 Top R&B/Hip hop albums
1996 Bow Down #2 #1 Platinum (1,700,000 copies)
2003 Terrorist Threats #16 #3 Gold (679,000)

Single zao

hariri
Mwaka Jina Chati iliyoshika[8] Albamu
Billboard Hot 100 Hot R&B/Hip-Hop Songs Hot rap singles
1996 "Bow Down" #21 #19 #1 Bow Down
1997 "Gangstas Make the World Go Round" #40 #30 #10
2002 "It's The Holidaze" - - - Friday After Next
2003 "Gangsta Nation" #33 #22 #9 Terrorist Threats

Marejeo

hariri
  1. "Mack 10 interview". AllHipHop.com. 10 Novemba 2005. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-07. Iliwekwa mnamo 2007-10-23.
  2. url=http://www.hiphopdx.com/index/features/id.1201/title./p.1 Archived 19 Septemba 2008 at the Wayback Machine.
  3. "Westside Connection chart history". Billboard. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-06. Iliwekwa mnamo 2007-09-12.
  4. Terrorist Threats. Allmusic. Retrieved on 2007-09-12.
  5. "Westside Connection certifications". RIAA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-01-03. Iliwekwa mnamo 2007-11-02.
  6. "Westside Connection information". FindArticles.com. 27 Septemba 2003. Iliwekwa mnamo 2007-09-12.
  7. "Westside Connection". MTV.com. 25 Machi 2004. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-01. Iliwekwa mnamo 2007-09-12.
  8. Westside Connection singles chart history. Billboard. Archived from the original on 2008-12-27. Retrieved on 2007-09-12.

Viungo vya nje

hariri