[go: up one dir, main page]

Vietnam

Nchi katika Asia ya Kusini-Mashariki


Vietnam (Việt Nam - 越南) ni nchi ya Asia ya Kusini-Mashariki.

Cộng hòa Xã hội Chủ nghĩa Việt Nam 共和社會主義越南
Jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam
Bendera ya Vietnam Nembo ya Vietnam
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: 獨立自由幸福 Độc lập – Tự do – Hạnh phúc
(Uhuru, Huria, Heri)
Wimbo wa taifa: Tiến Quân Ca
Lokeshen ya Vietnam
Mji mkuu Hanoi
21°2′ N 105°51′ E
Mji mkubwa nchini Mji wa Ho Chi Minh (Saigon)
Lugha rasmi Kivietnam
Serikali Jamhuri, chama kimoja 1
Tô Lâm
Lương Cường
Phạm Minh Chính
Uhuru
Kutoka China
(mapigano ya Bach Dang)
Kutoka Ufaransa
Ilitambuliwa

938

2 Septemba 1945
1954
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
332,698 km² (ya 65)
6.4
Idadi ya watu
 - Julai 2014 kadirio
 - 1999 sensa
 - Msongamano wa watu
 
90,630,000 (ya 13)
76,323,173
273.11/km² (ya 46)
Fedha Dong ya Vietnam (₫) (VND)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+7)
(UTC+7)
Intaneti TLD .vn
Kodi ya simu +84

-


Imepakana na China, Laos na Kambodia.

Mji mkuu ni Hanoi lakini mji mkubwa ni Mji wa Ho Chi Minh (zamani: Saigon).

Jiografia

hariri

Umbo la nchi ni kama kanda ndefu kando ya mwambao wa Bahari ya Kusini ya China. Umbali kati ya kaskazini na kusini ni km 1,650. Upana wa nchi kati ya mashariki na mipaka ya magharibi hutofautiana: kaskazini ni km 600, lakini kwenye shingo jembamba la Vietnam ya kati ni kilomita 50 tu. Pwani ina urefu wa km 3,000.

 
Kidaka cha Halong katika Vietnam Kaskazini.

Umbo la kijiografia limewahi kulinganishwa na "fimbo linalobeba mabakuli mawili": kaskazini na kusini kuna delta mbili za mto Mekong na Mto Mwekundu zenye rutuba; katikati nchi nyembamba ya milima na misitu.

Kuna maeneo makubwa matano:

Historia

hariri

Nchi ilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe.

Milki jirani ya China

hariri

Vietnam ilitawaliwa kwa karne kadhaa kutoka China kuanzia karne ya 2 KK. Athira ya utamaduni wa China ilibaki muhimu hata katika uhuru.

Katika karne ya 18 nchi iliunganishwa chini ya makaisari wa mji wa Hue.

Koloni la Ufaransa

hariri

Athira ya Ufaransa ilikua na kati ya miaka 1858 na 1883 utawala wa nchi ulichukuliwa na Ufaransa. Kusini mwa nchi kulikuwa koloni la Ufaransa kwa jina la Cochinchina. Annan (eneo la Vietnam ya Kati) na Tongking (kaskazini) zilikuwa nchi lindwa chini ya utawala wa kaisari wa Hue lakini hali halisi mamlaka ilikuwa mikononi mwa Ufaransa.

 
Hekalu la Kibuddha

Vita vya ukombozi

hariri

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Vietnam ilitwaliwa na Japani iliyoacha maafisa Wafaransa wa serikali ya Víchy ofisini lakini kushika utawala wa juu.

Kundi la Viet Minh walioongozwa na mkomunisti Ho Chi Minh waliwapinga kwa njia ya vita ya msituni.

Mwaka 1945 Japani ilijaribu kutumia Wavietnam upande wake ukaondoa Wafaransa madarakani na kumtangaza Kaisari Bao Dai wa Hue mtawala wa Vietnam huru.

Lakini baada ya miezi michache vita ikaisha na Ho Chi Minh alitangaza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam mjini Hanoi. Wafaransa wa serikali ya Paris walijaribu kujenga uhusiano naye lakini baada ya kurudi walilenga kuchukua utawala upya.

Vita vya kupigania uhuru vilifuata hadi mwaka 1954 Ufaransa ukashindwa.

Kipindi cha Vietnam mbili

hariri

Vietnam iligawiwa katika Vietnam Kaskazini na Vietnam Kusini. Jeshi na watawala wa kikoloni wa Ufaransa waliondoka kabisa. Wavietnam wengi wa kaskazini, hasa Wakristo, walioogopa serikali ya kikomunisti walikimbilia kusini.

Lakini uchaguzi huru uliokubaliwa huko Geneva haukutekelezwa kwa sababu serikali za kidikteta za kusini zilikataa.

Vita ya wenyewe kwa wenyewe ilianzishwa na wakomunisti wa kaskazini waliosaidiwa na China na Umoja wa Kisovyeti dhidi ya serikali ya kusini iliyopata msaada wa Marekani.

Kaskazini kuteka Kusini na kuunganisha taifa

hariri

Katika vita ya Vietnam majeshi ya Marekani na Vietnam Kusini yalishindwa.

Tarehe 30 Aprili 1975 jeshi la Vietnam Kaskazini lilitwaa mji wa Saigon. Nchi yote iliunganishwa kama Jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam tarehe 2 Julai 1976.

Nchi ilianza kubadilika mwaka 1986 kwa kuanza mahusiano na nchi zisizo za kikomunisti, na tangu hapo imepata maendeleo makubwa.

 
Wanawake katika soko la Hanoi, Vietnam

Kwa jumla kuna wakazi milioni 95.5.

Wengi (85.7%) ni Waviet. Wengine ni wa makabila madogomadogo 53 ambayo hakuna linalofikia 2%.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiviet.

Upande wa dini, siasa ya ukomunisti inabana uhuru lakini wanaozifuata wanaongezeka. Kadiri yake 26.8% tu za wakazi wamejiandikisha kufuata dini fulani, wakiwemo Wabuddha (12.2%), Wakatoliki (6.8%), Wakaoda (4.8%), waumini wa Hòa Hảo (1.4%) na Waprotestanti (1.5%), kumbe wengine wote hawamuamini Mungu.

Lakini utafiti kutoka nje unataja namba tofauti, hasa kwa dini za jadi, kwamba zinafuatwa na 45.3% za wakazi wote, na kwamba wasio na dini yoyote ni 29.6% tu.

Siasa na Uongozi

hariri

Kulingana na katiba ya nchi ya Vietnam, kipengele cha nne, chama cha siasa kinachotambulika ni Chama cha Kikomunisti cha Vietnam ambacho kina mamlaka juu ya majeshi, vyombo vya mawasiliano na nchi yote kwa ujumla. Vyama au makundi ya watu wanaotaka kuwa katika uchaguzi lazima yawe yameambatanishwa na chama hicho cha Kikomunisti. Kwa kawaida, watu na vyombo vya habari katika nchi hii hukiita chama hiki Đảng yaani 'chama chetu'.

Bunge la nchi hii ina wabunge 498. Bunge hii ina nguvu juu ya serikali na mahakama. Mawaziri wa nchi huchaguliwa kutoka kwa hili bunge. Bunge huongozwa na mwenyekiti

Mfumo wa mahakama

hariri

Mfumo wa mahakama wa Vietnam waongozwa na The Supreme People's Court of Vietnam na huongozwa na jaji mkuu. Hata hivyo, mfumo huo wa mahakama huwa chini ya bunge. Mahakama ya rufaa ndiyo kubwa sana nchini humo, chini yake kuna mahakama za jimbo na mahakama nyingine nyingi za mitaani. Mahakama ya kijeshi huwa na nguvu wakati nchi ilipo matatani.

Vietnam bado inakubali adhabu ya kifo na kulingana na makala ya Washington Post Archived 2014-02-12 at Archive.today, mwaka 2014, watu mia sababu walikuwa wauliwe kwa makosa mbalimbali.

Serikali

hariri

Rais wa Vietnam huwa ni mkuu wa nchi, kamanda mkuu wa jeshi na mwenyekiti wa baraza la Supreme Defense and Security. Waziri mkuu (Prime Minister ) wa Vietnam huwa mkuu wa baraza la mawaziri na tume zote za nchi.

Uchumi

hariri

Kati ya miaka 1940 na 1975 Vietnam ilikuwa na kipindi kirefu cha vita ikaonekana kama nchi maskini sana.

Tangu miaka ya 1980 uchumi umesonga mbeleː sasa ni kati ya nchi kwenye njia ya maendeleo zenye uchumi imara sana unaokua haraka.

Utalii

hariri

Utalii ni mojawapo ya nyanja ambazo zinachangia uchumi wa Vietnam. Tangu mwaka 2014, mji wa Hanoi umekuwa ukisifika na kupewa taji na tovuti ya Trip Advisor kuwa kati ya miji mizuri zaidi ya kusafiri duniani.

Vita vya Vietnam pia huchangia katika kufanya nchi hii inoge na kupata watalii wengi. Kuna mahala kama First Indochina War na Second Indochina War ambayo huonekana kama kivutio murua cha Vietnam. Pia The Imperial Citadel of Hue ni kivutio kingine cha watalii wanaotaka kuona kwenye vita za Vietnam zilifanyika.

Usafiri

hariri

Usafiri wa Vietnam, Vietnam tours huwa sanasana kwa ndege ambapo serikali imejenga nyanja za ndege. Pia kumekuwa na usafiri kwa kutumia pikipiki ambayo yafana sana. Nyanja za ndege za kimataifa ni:

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
Serikali
Vyombo vya habari na uhuru wa uandishi
Utalii
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Vietnam kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.