[go: up one dir, main page]

Rimegepanti (Rimegepant), inayouzwa kwa jina la chapa Nurtec ODT, ni dawa inayotumika kutibu na kuzuia kipandauso.[1] Inachukuliwa kwa mdomo.[2] Huanza kazi ndani ya masaa mawili na athari zake zinaweza kudumu kwa masaa 48.[3]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu na maumivu ya tumbo.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito na kunyonyesha hauko wazi.[4] Dawa hii inafanya kazi kwa kuzuia kipokezi cha CGRP.[2]

Rimegepanti iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2020.[2] Nchini Marekani, inagharimu takriban dola 120 za Marekani kwa kila dozi kufikia mwaka wa 2021.[5] Kufikia mwaka wa 2021 ilikuwa bado haijaidhinishwa Ulaya wala Uingereza.[6]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 "Nurtec ODT - rimegepant sulfate tablet, orally disintegrating". DailyMed. 19 Februari 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 19 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 "Rimegepant Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Skidmore-Roth, Linda (1 Aprili 2021). Mosby's Drug Guide for Nursing Students with 2022 Update - E-Book (kwa Kiingereza). Elsevier Health Sciences. uk. 1218. ISBN 978-0-323-87656-8. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Rimegepant (Nurtec ODT) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Nurtec ODT Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Juni 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Rimegepant". SPS - Specialist Pharmacy Service. 5 Oktoba 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rimegepanti kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.