[go: up one dir, main page]

Orodha ya milima mirefu duniani

Urefu wa mlima au kimo chake unaweza kukadiriwa kwa njia mbalimbali.

Mlima Everest ukitazamiwa kutoka upande wa kaskazini

Mbinu inayotumika mara nyingi ni kutaja tofauti kati ya usawa wa bahari na kimo cha kilele cha mlima. Lakini inawezekana pia kutumia mbinu tofauti zitakazoleta matokeo tofauti.

Mlima mrefu kutoka usawa wa bahari

hariri

Mlima mrefu duniani kwa kuangalia kimo juu ya uwiano wa bahari ni Mlima Everest ulioko kwenye mpaka baina ya Nepal na China. Kilele chake kipo mita 8,848 juu ya usawa wa bahari. Mlima Everest ni sehemu ya milima ya Himalaya. Pamoja na Everest kuna milima mingine 13 inayopita kimo cha mita 8,000, yote iko katika Himalaya na milima jirani ya Karakoram ambayo ni tokeo la kukunjwa kwa ganda la dunia tangu bamba la Uhindi lilianza kugonga bamba la Ulaya-Asia.

Nafasi Kilele Mita juu ya usawa wa bahari Milima Nchi
1. Mlima Everest
(Kitibet Chomolungma, Kinepali Sagarmatha)
&0000000000008848.0000008,848 Himalaya Nepal, China (Tibet)
2. K2 (Kichina Chogir) &0000000000008611.0000008,611 Karakoram Pakistan, China (Xinjiang)
3. Kangchenjunga &0000000000008586.0000008,586 Himalaya Uhindi (Sikkim), Nepal
4. Lhotse &0000000000008516.0000008,516 Himalaya Nepal, China (Tibet)
5. Makalu &0000000000008485.0000008,485 Himalaya Nepal, China (Tibet)

Mlima mrefu kutoka kitovu cha Dunia

hariri
 
Chimborazo

Kwa kutumia kitovu cha Dunia kama marejeo, yaani umbali kati ya nukta ya kitovu cha Dunia na kilele cha mlima, matokeo ni tofauti. Hapo mlima Chimborazo nchini Ekwador inafikia umbali wa kilomita 6,384.557 ikizidi Everest yenye km 6,382.414 kwa kilomita mbili.

Tofauti inasababishwa na umbo la Dunia ambalo si tufe kamili. Maana kuzunguka kwa Dunia kwenye mhimili wake unasababisha kani kitovu (kwa Kiingereza centripetal force) inayofanya umbo la Dunia kufanana kidogo na duaradufu. Hivyo umbali kutoka kitovu cha Dunia hadi ikweta ni mkubwa kiasi cha kilometa 43 kuliko umbali baina ya kitovu na ncha za Dunia.

Kwa kutumia marejeo hayo Mlima Everest una nafasi ya sita tu kati ya milima ya Dunia, ilhali milima kadhaa iliyopo karibu na ikweta inasogea mbele, kama milima katika Andes na mlima Kilimanjaro nchini Tanzania.

Nafasi Mlima Kimo juu ya
kitovu cha Dunia
kwa mita
Mita juu ya
usawa wa bahari
Nchi
1. Chimborazo 6,384.557 &0000000000006267.0000006,267 Ekwador
2. Huascaran 6,384.552 &0000000000006768.0000006,768 Peru
3. Cotopaxi 6,384.190 &0000000000005897.0000005,897 Ekwador
4. Kilimanjaro 6,384.134 &0000000000005895.0000005,895 Tanzania
5. Cayambe 6,384.094 &0000000000005796.0000005,796 Ekwador
6. Mount Everest 6,382.414 &0000000000008848.0000008,848 Nepal

Mlima mrefu kutoka mguu wake

hariri

Njia nyingine ni kupima ni kiasi gani mlima unainuliwa juu ya mazingira yake yaani pale inapoanza kuonekana. Kwa kutumia marejeo hayo mlima mrefu kabisa duniani ni Mauna Kea. Volkeno hii inayofanya kisiwa kizima kimojawapo cha funguvisiwa la Hawaii inaanza mita 6,000 chini ya uso wa bahari na kufikia mita 4,205 juu ya usawa wastani wa bahari, hivyo kimo chake kutoka mguu wake hadi kilele ni mita 10,203[1]

Kati ya milima inayoinuliwa juu ya mazingira ya nchi kavu iko

Mlima mrefu katika Mfumo wa Jua

hariri

Kwenye sayari na miezi ya mfumo wa Jua letu kuna milima mikubwa zaidi kuliko duniani. Mlima mkubwa unaojulikana hadi sasa ni Olympus Mons kwenye Mirihi (Mars). Volkeno hii inapanda kilomita 26 juu ya tambarare ya mazingira yake ikiwa na kipenyo cha kilomita 600. Kasoko kwenye kilele chake ina kipenyo cha kilomita 80.

Tanbihi

hariri
  1. Highest Points on Earth, tovuti ya National Geographic, iliangaliwa 14 Januari 2014