[go: up one dir, main page]

Nikaragua (pia Nikaragwa) ni nchi ya Amerika ya Kati yenye wakazi 6,071,045 (2012). Imepakana na Honduras na Kosta Rika; upande wa magharibi ni pwani ya Pasifiki na upande wa mashariki kuna pwani ya Bahari ya Karibi.

República de Nicaragua
Jamhuri ya Nikaragua
Bendera ya Nikaragua Nembo ya Nikaragua
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Pro Mundi Beneficio
(Kilatini: Kwa salama ya dunia)
Wimbo wa taifa: Salve a ti, Nicaragua
(Usalimiwe Nikaragua)
Lokeshen ya Nikaragua
Mji mkuu Managua
12°9′ N 86°16′ W
Mji mkubwa nchini Managua
Lugha rasmi Kihispania (kitaifa) (Kiingereza, lugha 6 za kienyeji kimahali kwenye pwani ya Karibi)
Serikali Jamhuri
Daniel Ortega
Uhuru
Imetangazwa
Imetambuliwa

15 Septemba 1821
25 Julai 1850
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
130,000 km² (ya 97)
14.01
Idadi ya watu
 - Julai 2012 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
6,071,045 (ya 108)
51/km² (ya 155)
Fedha Cordoba (NIO)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-6)
(UTC)
Intaneti TLD .ni
Kodi ya simu +505

-



Ramani ya Nikaragua

Jina la nchi linasemekana kuwa mchanganyiko wa jina la wakazi asilia walioitwa "Nikarao" na neno la Kihispania la "agua" (=maji) kutokana na maziwa makubwa mawili nchini yanayoitwa Lago Managua na Lago Nicaragua. Maelezo mengine yanamtaja chifu wa wazalendo wakati wa kufika kwa Wahispania aliyeitwa "Nikarao".

Jiografia

hariri

Nikaragua ina volkeno nyingi; nyororo ya milima ya kivolkeno hufuata mstari wa pwani ya Pasifiki.

Sehemu ya juu ni mlima Mogoton wenye kimo cha mita 2,438 juu ya UB.

Maziwa makubwa mawili ya maji matamu ni Lago Managua na Lago Nicaragua.

Eneo upande wa Karibi lina wakazi wachache sana: ni hasa eneo la misitu minene.

Historia

hariri

Nchi ilikuwa koloni la Hispania tangu mwaka 1524.

Mwaka 1821 iliachana na utawala wa Hispania pamoja na nchi jirani na kuingia katika Shirikisho la Amerika ya Kati.

Tangu mwaka 1854 imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.

Wakazi

hariri

Wakazi walio wengi sana hukalia maeneo ya mji mkuu Managua na pwani ya Pasifiki.

Sehemu kubwa (69 %) ni machotara kati ya wakazi asilia na Wazungu. 7% ni Wazungu. 9% wana asili ya Afrika, wakikaa hasa kwenye pwani Ya Bahari ya Karibi. Waindio ni asilimia 5.

Lugha rasmi na kubwa zaidi ni Kihispania, lakini si lugha pekee.

Upande wa dini, walio wengi ni Wakatoliki (61.5% kadiri ya sensa ya mwaka 2005) na Waprotestanti (30.6%). 15.1% hawana dini yoyote.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Taarifa za jumla
Sanaa na utamaduni
Mengineyo
  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nikaragua kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

13°N 85°W / 13°N 85°W / 13; -85