Mikoa ya Italia
Mikoa ya Italia ni vitengo vikuu vya utawala chini ya ngazi ya taifa nchini. Eneo lote la Italia limegawiwa katika mikoa 20. Kila mkoa huwa na kiwango cha madaraka cha kujiamulia, lakini mikoa 5 huwa na madaraka ya kujitawala. Madaraka hayo na kuwepo kwa kila mkoa yameandikwa katika katiba ya nchi.
Kila mkoa - isipokuwa ule wa Bonde la Aosta - hugawiwa katika wilaya.
Madaraka ya mikoa ya kawaida na mikoa ya kujitawala
haririKikatiba kila mkoa huwa na madaraka ya kujiamulia kuhusu mambo pasipo sheria ya kitaifa na katika mambo yafuatayo:
- kupokea kiwango cha kodi (takriban 20%) kwa kulipia madhumuni ya mkoa
- kutawala shule, usafiri wa umma na hospitali mkoani
- kufanya uchaguzi wa bunge na serikali ya kimkoa.
Mikoa mitano ya kujitawala huwa na madaraka makubwa zaidi yanayotofautiana kati ya mkoa na mkoa. Sababu za haki hizo za pekee ni za kihistoria na kuwepo kwa sehemu za wananchi wenye lugha mama tofauti na Kiitalia. Mikoa hii ni Bonde la Aosta (Kiitalia-Kifaransa), Friuli-Venezia Giulia (Kiitalia-Kifurlan-Kislovenia), Sardinia (Kisardinia), Sisili na Trentino-Alto Adige/Südtirol (Kiitalia - Kijerumani).
Mikoa hii inaitwa "mikoa yenye sheria za pekee"; kwa mfano Friuli-Venezia Giulia inabaki na asilimia 60 za kodi kutoka eneo lake, Sardinia na 70%, Trentino-Alto Adige/Südtiro pamoja na Aosta zinashika 90% na Sisili inashika kodi zote chini ya mamlaka ya kimkoa.
Orodha ya mikoa
haririBendera | Jina | Makao makuu | Eneo (km2) | Wakazi | Msongamano wa watu/km² | Wilaya | Miji | Miji mikubwa | Hali ya utawala |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Abruzzo | L'Aquila | 10,763 | 1,307,919 | 122 | 4 | 305 | - | Kawaida | |
Bonde la Aosta | Aosta | 3,263 | 126,933 | 39 | 0 | 74 | - | Kujitawala | |
Apulia | Bari | 19,358 | 4,045,949 | 209 | 6 | 258 | Bari | Kawaida | |
Basilicata | Potenza | 9,995 | 575,902 | 58 | 2 | 131 | - | Kawaida | |
Calabria | Catanzaro | 15,081 | 1,954,403 | 130 | 5 | 409 | Reggio Calabria | Kawaida | |
Campania | Napoli | 13,590 | 5,761,155 | 424 | 5 | 551 | Napoli | Kawaida | |
Emilia-Romagna | Bologna | 22,446 | 4,354,450 | 194 | 9 | 348 | Bologna | Kawaida | |
Friuli-Venezia Giulia | Trieste | 7,858 | 1,219,356 | 155 | 4 | 218 | Trieste | Kujitawala | |
Lazio | Rome | 17,236 | 5,550,459 | 322 | 5 | 378 | Rome | Kawaida | |
Liguria | Genoa | 5,422 | 1,565,349 | 289 | 4 | 235 | Genoa | Kawaida | |
Lombardia | Milan | 23,861 | 9,749,593 | 409 | 12 | 1544 | Milan | Kawaida | |
Marche | Ancona | 9,366 | 1,541,692 | 165 | 5 | 239 | - | Kawaida | |
Molise | Campobasso | 4,438 | 312,394 | 70 | 2 | 136 | - | Kawaida | |
Piemonte | Turin | 25,402 | 4,366,251 | 172 | 8 | 1206 | Turin | Kawaida | |
Sardinia | Cagliari | 24,090 | 1,637,193 | 68 | 8 | 377 | Cagliari | Kujitawala | |
Sisilia | Palermo | 25,711 | 4,994,817 | 194 | 9 | 390 | Catania, Messina, Palermo | Kujitawala | |
Trentino-Alto Adige/Südtirol | Trento | 13,607 | 1,036,707 | 76 | 2 | 333 | - | Kujitawala | |
Toscana | Firenze | 22,994 | 3,679,027 | 160 | 10 | 287 | Firenze | Kawaida | |
Umbria | Perugia | 8,456 | 885,535 | 105 | 2 | 92 | - | Kawaida | |
Veneto | Venisi | 18,399 | 4,865,380 | 264 | 7 | 581 | Venisi | Kawaida |