Jamii kunde
(Elekezwa kutoka Makundekunde)
Jamii kunde (makundekunde) ni jina la kujumlisha mbegu za kuliwa zinazofanana na kunde. Zote zinatokana na mimea ya jamii ya Fabacea (au Leguminosa). Mbegu hizi ziko ndani ya ganda linalokauka na kumwaga mbegu kwa ardhi.
Mbegu za makundekunde ni sehemu muhimu ya chakula cha kibinadamu kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini na pia huleta mazao mazuri. Kwa watu wasiokula nyama au wana uwezo mdogo tu kujipatia nyama mbegu za jamii kunde zinatosheleza mahitaji ya protini.
Kati ya mazao ya jamii kunde ni:
- bwanda
- choroko
- dengu
- fiwi
- fiwi mafuta au njahe
- gwaru
- maharagwe
- kunde
- kunde-mwitu
- mbaazi
- njegere kubwa
- njegere za kizungu
- njugu au karanga
- njugu-mawe
- njugu Hausa
- soya
-
Bwanda
-
Choroko kijani
-
Aina za dengu
-
Fiwi
-
Fiwi mafuta
-
Gwaru
-
Maharagwe
-
Kunde
-
Kunde-mwitu
-
Mbaazi
-
Njegere kubwa
-
Njegere za kizungu katika ganda
-
Njugu
-
Njugu-mawe
-
Soya katika ganda
-
Aina za soya