Kikohozi
Kikohozi ni kitendo cha ghafla na kinachojirudiarudia kama sehemu ya mwili kukabiliana na vitu vigeni na vijidudu vya magonjwa katika njia ya hewa. Tunakohoa ili kuondoa vitu hivyo vitoke kwenye njia ya hewa.
Kijana mdogo akikohoa sababu ya pertussis ugonjwa unaosababisha Kifaduro.
|
Kitendo cha kukohoa kimegawanyika katika awamu tatu:
- Kuvuta hewa,
- Kutoa hewa kwa nguvu dhidi ya koo (glota) lilofungwa,
- kutoa hewa kwa kasi kutoka kwenye mapafu baada ya kufunguka kwa glota, kwa kawaida hutoka kwa sauti isiyo ya kawaida.[1] Kikohozi kinaweza kuwa tendo la hiari au lisilo hiari.
Kikohozi cha mara kwa mara kinaashiria kuwa kuna ugonjwa. Virusi na bakteria wengi humsababishia mtu kikohozi. Mtu huyo mwenye maambukizi akikohoa huwasambazia wengine ugonjwa. Mara nyingi, kikohozi kisicho cha kawaida kinasababishwa na maambukizi katika njia ya hewa, lakini kinaweza kusababishwa na kitu chochote kinachoweza kuziba njia ya hewa, uvutaji sigara, uchafuzi wa hewa, pumu, magonjwa ya kiungulia, makamasi yanayotiririka kwa ndani ya pua, bronkaitisi sugu, uvimbe wa mapafu, moyo kushindwa kufanya kazi na matumizi ya dawa kama ACE inhibitors.
Tiba ya kikohozi ni sharti ilekezwe dhiti ya kisababishi; kwa mfano, kuacha kuvuta sigara au kuacha kutumia ACE inhibitors.
Dawa za kutuliza kikohozi kama vile codeine au dextromethorphan hupendekezwa sana, lakini zimekuwa na mchango mdogo. Kwa upande mwingine matibabu yanaweza kulainisha kikohozi na kuzalisha makohozi. Kama ilivyo njia asilia ya mwili kujikinga, kutuliza kikohozi kunaweza kuleta madhara ya uharibifu, hasa pale kikohozi kinapokuwa kinazalisha makohozi.[2]
Kinavyotokea
haririMagonjwa ya ziada
haririMagonjwa ya ziada yanayosababishwa na kikohozi yanaweza kuwa ya muda mfupi au ya muda mrefu (sugu).
Ya muda mfupi ni pamoja na kuzimia kwa sababu ya kupungua kwa damu kwenye mzunguko wa ubongo kikohozi kinapokuwa cha muda mrefu na kukohoa kwa nguvu, kukosa usingizi, kutapika sababu ya kikohozi, kutokwa na haja kubwa au mkojo wakati wa kukohoa.
Magonjwa ya muda mrefu ni pamoja na kupata madhara kwenye misuli ya fupanyonga na hata kwenye kibofu cha mkojo.[3]
Tanbihi
hariri- ↑ Chung KF, Pavord ID (Aprili 2008). "Prevalence, pathogenesis, and causes of chronic cough". Lancet. 371 (9621): 1364–74. doi:10.1016/S0140-6736(08)60595-4. PMID 18424325.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Pavord ID, Chung KF (Aprili 2008). "Management of chronic cough". Lancet. 371 (9621): 1375–84. doi:10.1016/S0140-6736(08)60596-6. PMID 18424326.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Cystocele (Prolapsed Bladder) | NIDDK", National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. (en-US)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kikohozi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |