Kiafrikana
Kiafrikana au Kiafrikaans ni lugha ya Afrika Kusini iliyotokea katika karne nne zilizopita kwenye msingi wa Kiholanzi pamoja na athari za lugha mbalimbali. Hata kama ni lugha iliyozaliwa Afrika na kujadiliwa hapa, kitaalamu ni kati ya lugha za Kijerumaniki.
Imekuwa lugha rasmi katika Afrika Kusini tangu mwaka 1925 badala ya Kiholanzi. Hadi sasa ni lugha rasmi mojawapo Afrika Kusini pamoja na lugha 9 nyingine. Ni pia kati ya lugha za taifa huko Namibia.
Kiafrikana kina wasemaji wa lugha ya kwanza milioni saba ambao ni sawa na 13.5% za raia wa Afrika Kusini, ambako ni lugha ya tatu wenye wasemaji wengi baada ya Kizulu na Kixhosa.[1] Wasemaji wote hukadiriwa kuwa kati ya milioni 15 hadi 23.
Ni lugha kuu kwenye nusu ya magharibi ya Afrika Kusini yaani kwnye majimbo ya Rasi ya Kaskazini na Rasi ya Magharibi. Kufuatana na sensa ya 2011 wasemaji wa Kiafrikana ni Machotara wa Afrika Kusini milioni 4.8, Wazungu wa Afrika Kusini milioni 2.7, Waafrika Weusi 600,000 na Wahindi wa Afrika Kusini 58,000.
Kiasili kilianzisha kutokana na Kiholanzi cha makaburu wa kwanza kikapokea asilimia 5-10 za msamiati kutoka lugha za Khoikhoi, Wareno, Wabantu, Wajerumani, Wafaransa na Waingereza. ya Afrika Kusini lakini imekuwa pia lugha ya wakazi chotara katika jimbo la Rasi Magharibi ("Cape Coloureds"). Leo hii wasemaji wa asili ya Ulaya ni chini ya nusu ya wasemaji wote wa Kiafrikana.
Tanbihi
- ↑ Census 2011: Census in brief (PDF). Pretoria: Statistics South Africa. 2012. uk. 27. ISBN 9780621413885. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 13 Mei 2015.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
- makala za OLAC kuhusu Kiafrikana Archived 19 Novemba 2014 at the Wayback Machine.
- lugha ya Kiafrikana katika Glottolog
- (en) Muhtasari kuhusu Kiafrikana kwenye Ethnologue
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiafrikana kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |