Bahari ya Kaspi
Bahari ya Kaspi (Kiarabu: بحر قزوين Baḥr Qazvin; Kiajemi: دريا خزر darya khazar; Kirusi: Каспийское море kaspiiskoye more) ni ziwa kubwa kabisa duniani lenye eneo la km² 371,000 na mjao wa km³ 78,200. Liko kati ya Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan na Uajemi.
Kimo chake kinafikia mita 1,025.
Huitwa "bahari" kwa sababu maji yake ni ya chumvi ingawa si kali sana kama ya bahari yenyewe.
Maji ya chumvi
haririUpande wa kaskazini inaingia mito miwili mikubwa ya Volga na Ural. Inasababisha kiasi kidogo cha chumvi upande huo wa kaskazini. Asilimia ya chumvi huonegezeka kuelekea kusini.
Madini
haririChini ya bahari kuna akiba kubwa za mafuta ya petroli na gesi, hasa karibu na Baku. Katika hori ya Kara-Bogas chumvi hulimwa.
Viungo vya Nje
hariri- Information on history and names of the Caspian Sea
- Caspian Sea Region
- Caspian Environment Programme
- Target: Caspian Sea Oil Archived 28 Agosti 2009 at the Wayback Machine. John Robb, 2004
- Dating Caspian sea level changes Archived 24 Julai 2011 at the Wayback Machine.